wa kijiji cha Nyangae, Kata ya Bukumbi
wilayani Uyui, Shimba Kajolo
ameburuzwa mahakamani akituhumiwa
kumnajisi binti yake wa miaka 12.
Imeelezwa mahakamani kwamba alifanya
kitendo hicho kwa kushauriwa na mganga
wa kienyeji ili aweze kuondoa mkosi wa
kutopata mke.
Kajolo amefikishwa mbele ya Hakimu
Mkazi wa Wilaya ya Tabora, Bahati
Chitepo na kusomewa shitaka lake hilo.
Mbele ya Hakimu Chitepo ilidaiwa na
Wakili wa Serikali, Miraji Kajiru kuwa
mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 11,
mwaka huu. Wakili Kajiru aliiambia mahakama kuwa
siku hiyo majira ya usiku Shimba
alimnajisi binti yake wa kumzaa (jina
linahifadhiwa).
Mtuhumiwa amekana shitaka hilo na
amepelekwa mahabusu baada ya kukosa
watu wa kumdhamini hadi Septemba tatu
kesi hiyo itakapotajwa.