Featured Posts

Thursday, August 28, 2014

POLISI AMGONGA MTOTO NA KUKIMBIA AKILITELEKEZA GARI

POLISI mmoja ambaye hakufahamika jina lake
mara moja, aliyekuwa akiendesha gari kwa
mwendo wa kasi, Jumapili iliyopita alimgonga
mtoto wa kike, Zahara Almeda katika barabara
ya Mji Mpya .
Mtoto Zahara Almeda aliyegongwa na polisi
huyo.
Katika tukio ambalo mwandishi wa habari hizi
alilishuhudia, mara tu baada ya kumgonga
mtoto aliyekuwa akitoka sokoni kununua
magimbi na mihogo , askari huyo aliteremka
na kukimbia akiliacha nyuma gari lake
lililokuwa bado halijazimwa , ambalo ndani yake
kulikuwa na kofia yake.
Polisi wa usalama barabarani akiwa eneo la
tukio .
Wananchi waliojawa na hasira baada ya tukio
hilo walilizingira gari hilo na kutaka kulichoma
moto , lakini busara za baadhi yao ziliwezesha
kitendo hicho kutofanyika na baadaye trafiki
alifika kudili na tatizo hilo
Mmoja wa watu walioshuhudia ajali hiyo
iliyolihusu gari aina ya Toyota Baloon lenye
namba za usajili T 5** AUE, alisema mtoto
aliyegongwa alikuwa akitokea sokoni Mji
Mpya , akiwa amebeba kikapu kichwani .
Mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sudi
Kiwamba , alisema binti huyo alikuwa
ameshavuka barabara , lakini wakati akijiandaa
kuvuka msingi wa pembeni gari hilo lilimfuata
katika jitihada za kumkwepa mwendesha
pikipiki.
Watu wakishuhudia tukio hilo.
Hata hivyo , siku moja baada ya tukio hilo,
mwandishi wetu alizungumza na baba mzazi
wa mtoto huyo alisema mwanaye anaendelea
vizuri na mtu aliyemgonga alikwenda
hospitalini kumjulia hali kwani aliamini alikuwa
amefariki .

TUMEAMIA HUKU