Featured Posts

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Sunday, August 31, 2014

BREAKING NEWZ; MADUKA KARIAKOO YAFUNGWA: SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

Picha hali Ilivyosasa kariakoo ambapo Wafanyabiashara wamefunga Maduka Yao ikidaiwa Kupinga matumizi ya mashine ya EFD..Hii ndo hali ilivyo asubuhi hii wafanyabiashara wa soko la kariakoo leo wamefunga maduka yao 



JAMANI ACHENI NUH MZIWANDA APAGAWE KWA SHILOLE, HATA AJICHORE TATOO HADI MATAK0N1 MIE



 


 


 

HATIMAYE UPEPO UMEGEUKA KAJALA SASA ANA PESA CHAFU, KUMUAJIRI WEMA,

AMA kweli fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, umekosea sana kwani upepo umegeuka, ungana na Ijumaa Wikienda.
Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
“Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya Sinza-Madukani jijini Dar.
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.
Pichani ni mjengo ambao Kajala Masanja amepanga.
KAJALA AMEHONGWA?
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.
WEMA HALI IPOJE?
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Gari la aina ya Toyota Brevis inayomilikiwa na Kajala.
Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa likiwemo la kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu ambalo ni Toyota Harrier.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
WEMA ATAFUTWA
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
SHOSTI WAKE
Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina gazetini, rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
“Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama ilivyokuwa zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye wakati ule alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akitafakari jambo.
KUMBUKUMBU YA JUZIKATI
Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
DIAMOND ALINENA
Baada ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
“Kama kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume, jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini jukumu la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond mtandaoni.

NOMA GARI LA MSANII DUDE LAIBUA MAZITO MAPYA KABISAA

Stori: Mayasa Mariwata
Kumbe! Lile gari aina ya Toyota Vitz la staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambalo hivi karibuni lilikamatwa kwa msala wa kuhusika na ujambazi jijini Dar, limeibua mapya likiwa bado linashikiliwa na polisi kwenye Kituo cha Kijitonyama a.k.a Mabatini.
Habari za kifukunyuzi zinadai kwamba ndinga hilo si mali ya Dude kama ilivyoelezwa awali, bali ni la mwanamke ‘anayechepuka’ naye aliyetajwa kwa jina moja la Lily ambaye eti ni mke wa mtu (Samson).
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu kutoka Meatu mkoani Simiyu, Samson ambaye ni mume wa Lily alisema alistaajabu aliposikia Dude akisema gari ni lake wakati ni la mkewe aliyefunga naye ndoa mwaka 2011 na yeye alishiriki kulinunua.
Gari aina ya Toyota Vitz la staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
“Huyo Dude anajua ukweli wa mambo, gari si lake, ni la mke wangu tena fedha ya kulinunulia haikutosha ikabidi nimuongezee laki nne kwa kuwa alikuwa akidaiwa kwa usumbufu mkubwa.
“Isitoshe katika vijana waliokamatwa na gari hilo, mmoja ni mdogo wa mke wangu na siri zote za yeye kutoka na Lily huwa ndugu zake wananisimulia.
“Mara kadhaa nimemuonya Dude lakini huwa anakana kuwa hatoki naye bali ukaribu wao ni kutokana na sanaa na kudai ni kama ndugu kwa kuwa alikuwa akijuana na mama yake,” alisema.
Baada ya madai hayo kuwa ‘hoti’, Ijumaa Wikienda lilimsaka Lily ambaye hakuwa tayari kuzungumza kama gari hilo ni lake au la Dude na kusisitiza aulizwe Dude ambaye alikiri kufahamiana naye huku akikubali kumfahamu Samson pia.
Kulwa Kikumba ‘Dude’ akiwa ndani ya ofisi za Global.
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Dude aliyekiri kuwafahamu Samson na Lily kuwa ni wanandoa japokuwa wana migogoro.
“Matatizo yao ya ndoa wasihamishie kwangu, gari ni langu na lilikuwa linauzwa, Lily nimemlea kisanii maana marehemu mama yake mzazi nilikuwa namuita dada, ndiye aliyenikabidhi Lily mwaka 2003.
“Nimejaribu kumsaidia kisanii, sitaki kuchafuka, Lily ni mwanangu nimemlea,” alisema Dude

WAREMBO KAMA NANE HIVI WACHEZEA KICHAPO KIKALI USIKU WA MANANE

Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
Imekaa poa sana! Miezi kadhaa baada ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers kufichua uchafu wa biashara haramu ya ngono kwenye Mtaa wa Mwanzo Mgumu, Kata ya Mwembesongo, maeneo ya Msamvu mjini hapa, warembo wanaojiuza eneo hilo wamekula kibano na malori yanayopaki mahali hapo yametimuliwa.
Baadhi ya machangu walionaswa wakijiuza.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, kiongozi wa mtaa huo, Said Omar Kamba alisema: “Kwanza nayapongeza magazeti ya Global (Publishers) kupitia kitengo chao cha OFM ambao walivamia Kambi ya ltingi (Msamvu) kwa kushirikiana na polisi na kuwafuma wanawake waliokuwa wakifanya biashara haramu ya kuuza miili na kutupa hovyo kondom ambazo watoto wa mtaani kwetu walikuwa wakiziokota na kupuliza wakidhani ni mapulizo, jambo ambalo ni hatari.
“Baada ya habari hiyo kuripotiwa na magazeti ya Global, tumewatimua wanawake wanaojiuza baada ya kuketi kikao cha Baraza Maalum la Kata ‘BMK’ na kukubaliana kwamba dawa yao ni kuyaondoa malori eneo hili la ltingi.
Machangu hawa walinaswa wakiwa katika chumba kimoja.
“Uchunguzi wetu ulibaini kwamba madereva na ‘mataniboi’ huwanunua wasichana hao na kufanya nao ngono kwenye malori na baadaye kutupa hovyo kondom, kimsingi eneo hili ni ‘rizevu’ ya barabara ya Tanroads na tumeshawasiliana nao juu ya uamuzi huo.”
Alipoulizwa malori hayo sasa yamehamishiwa wapi, kiongozi huyo alisema: “Tumeyatengea eneo la Njia-Panda ya Tungi nje kidogo ya Mji wa Morogoro.”

INAUMA SANA! MFANYABIASHARA AMCHARANGA MAPANGA ALBINO

Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
INAUMA sana! Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro likimshikilia mkazi wa wilayani Mvomero, Johnson Damian Mkude kwa msala wa kumchinja mdogo wake na kupeleka kichwa kwa mganga wa kienyeji ili awe bilionea, jeshi hilo linamshikilia mfanyabiashara mwingine maarufu mkoani hapa aitwaye Lyimo kwa tuhuma za kumcharanga mapanga Damas Valeniani (36) ambaye ni  mlemavu wa ngozi (albino).
Mlemavu wa ngozi Damas Valeniani aliyecharangwa mapanga na mfanyabiashara maarufu mkoani Morogoro anayefahamika kwa jina moja la Lyimo.
Jamaa huyo maarufu kwa jina la Mangi, anadaiwa kutenda unyama huo wiki iliyopita usiku wa manane kwenye Msitu wa Milima ya Uluguru, Mtaa wa Bingwa Kiwasi Juu, Kilakala, wakati mlemavu huyo, akiwa amelala.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mlemavu huyo alisema:
“Nilikuwa nimelala, ghafla nikasikia mtu akiingia akiwa ameshika panga na kuanza kunikatakata huku akitaka kuninyofoa masikio yangu. Nilimtambua kuwa ni Lyimo ambaye ni jirani yetu.”
Eneo la tukio ambalo Bw. Damas Valeniani alishambuliwa kwa mapanga.
Alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo, alijitetea vya kutosha na kufanikiwa kuchomoka, kwa bahati nzuri mpwa wake, Mathias John alitokea na kumsaidia huku wakipiga kelele za kuomba msaada lakini tayari alikuwa amshamcharanga panga kichwani na kusababisha atokwe na damu nyingi.
Alisema kuwa kutokana na woga alioupata, aliogopa kulala hivyo alikimbilia kwa mjumbe wa mtaa wao, Filemon Gyuna ambako alipatiwa huduma ya kwanza.
Dada wa Damas Valeniani.
“Kulipokucha ndipo tukaenda kuripoti polisi na kupewa jalada la kesi namba MOR/RB/5122/2014-SHAMBULIZI.
“Polisi walifika nyumbani na kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kwenye mkono wa sheria na mimi nikapewa PF-3 kwa ajili ya matibabu kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro,” alisema Damas kwa maumivu makali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SAC Leonard Paul akifafanua jambo.
Akihojiwa na mwandishi wetu juu ya tukio hilo, mwenyekiti wa mtaa huo, Ally Malekela alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba Lyimo alipewa saa 24 za kuhama kwenye mtaa huo.
Wananchi mbalimbali waliozungumza na Ijumaa Wikienda, walisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, SAC Leonard Paul, anatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kukabiliana na matukio kama hayo.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Mkoa wa Morogoro, David Mganga alisema: “Natoa wito kwa jamii ielewe kuwa kiungo cha albino hakiwezi kumpa mtu utajiri au mafanikio, waache kututesa sisi maalbino.”

MWIMBAJI WA TAARABU WA BONGO ANUSURIKA KUUAWA NA AL SHABAAB HUKO MOMBASA

Oooh nooo ! Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la
Mashauzi Classic , Aisha Ramadhani ‘ Isha
Mashauzi’ , amejikuta kwenye wakati mgumu
baada ya kuvamiwa na kundi linalojiita Al -
Shaabab ( siyo wale orijino wanaosifika kwa
ugaidi ).
Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi
Classic , Aisha Ramadhani ‘ Isha Mashauzi ’ .
Tukio hilo ambalo liliibua sintofahamu kwa
wananchi , lilitokea juzikati katika hoteli
inayojulikana kwa jina la Grassovila iliyopo
Mombasa nchini Kenya ambapo walimuibia
msanii huyo kila kitu alichokuwa nacho .
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Isha
alisema kuwa alikwenda Mombasa kwa ajili ya
mwaliko wa mashabiki wa Timu ya Arsenal ya
England waishio Mombasa na alipokuwa
akijiandaa hotelini, ghafla alishtukia watu
waliojificha nyuso wakiingia katika chumba
alichokuwepo kisha kumuamuru atoe kila kitu.
“ Nilishtuka sana kuona kundi la watu likivamia
chumbani kwangu , nasikia walianzia katika
vyumba vingine , jamaa walinichukulia kila kitu
nilichokuwa nacho hadi hati ya kusafiria lakini
namshukuru Mungu Watanzania wenzangu
walinisaidia na kuweza kurejea Bongo,”
alisema Isha .
Alisema polisi nchini humo wanaendelea
kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuwatia hatiani
‘ wahuni’ hao.
Hadi Isha anafanikiwa kurudi Bongo, hakuna
mtu yeyote ambaye alikamatwa kuhusiana na
tukio hilo.

KUHUSU TUUMA ZA KUMRISHA DIAMOND VIPORO KILA SIKU.. WEMA AFUNGUKA .. SOMA HAPA ALICHOJIBU

MAHABATi ! Beautiful Onyinye wa Bongo,
Wema Sepetu ‘ Madam’ amedhihirisha kuwa
yeye ni mwanamke tayari wa kuwekwa ndani
baada ya kusema anajitahidi kila siku katika
suala la mapishi ili asimlishe viporo mwandani
wake, Nasibu Abdul , ‘ Diamond’ . Akipiga domo na paparazi wetu , Wema
alisema kama mwanamke anajua thamani ya
mwanaume siku zote hata kama ‘ baby ’ wake
atarudi usiku , lazima aingie jikoni kupika na
haweki chakula kwenye ‘ hot pot ’ .
“ Siku zote si kwamba najisifia ila kwa jikoni
ndiyo mwenyewe sasa kwa nini nipike chakula
halafu niweke kwenye hot pot ? Kwangu
siruhusu kabisa itokee , ” alisema Wema .

HII KALI. WAZIRI MKUU PINDA AWAKIMBIA WAANDISHI WA HS

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda jana
alilazimika kutumia mlango wa uani
kuondokea badala ya ule mkuu kwa kile
kinachohisiwa kuwakwepa waandishi wa
habari waliokuwa wakifuatilia ufunguzi
wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya
nje na mazingira kutoka nchi za Afrika.
Pinda ambaye alikuwa akifungua
mkutano huo, aliondoka mara tu baada ya
kumaliza shughuli iliyompeleka huku
akiacha kushiriki tukio la kupiga picha
lililoandaliwa kwa ajili yake upande wa
lango kuu wa ukumbi huo ambako
waandishi walikuwa wakimsubiri kwa
ajili ya kufanya naye mahojiano.
Awali wakati Pinda akihutubia mkutano
huo uliokuwa ukifanyika katika Ukumbi
wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,
baadhi ya maofisa wa itifaki walionekana
wakisimamia zoezi la kupanga viti kwa
ajili ya tukio la picha ya pamoja ambalo
Waziri Mkuu huyo kama mgeni rasmi
ilitakiwa ashiriki.
Ni maofisa hao pamoja na baadhi ya
watumishi wa idara zinazohusika na
mkutano huo, ndio waliowaelekeza
baadhi ya waandishi wa habari ambao
hawakubahatika kuingia ndani kusubiri
katika eneo hilo la lango kuu ili waweze
kufanya mahojiano na Pinda hata hivyo
ahadi hiyo haikutimia.
Hatua hiyo ndiyo iliyoibua hisia kwamba
huenda, Pinda alifanya hivyo kukwepa
maswali ya waandishi wa habari hasa
kutokana na kuwepo kwa taarifa
zinazodai kuwa ametangaza dhamira yake
ya kuwania ukuu wa dola mwaka 2015.
Tangu taarifa hizo ziripotiwe kwa mara ya
kwanza na vyombo vya habari Jumapili
iliyopita, si Pinda wala wasaidizi wake wa
karibu ambao walijitokeza kuthibitisha
juu ya taarifa hizo.
Kutokana na hilo vyombo vya habari
nchini vimekuwa vikimtafuta Pinda ili
aweze kuzungumzia habari hizo, ambazo
anadaiwa kuzitoa mbele ya wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Taifa kutoka mikoa ya Kanda ya
Ziwa aliokutana nao Ikulu ndogo ya jijini
Mwanza, Jumamosi iliyopita.
Katika tukio la jana wakati waandishi
wakimsubiri nje ya lango kuu, Pinda
alionekana akishuka chini na kuingia
katika eneo la pembeni ya ukumbi,
ambako inasemekana eneo hilo lina
mlango wa nyuma wa kutokea nje ya
ukumbi.
Waandishi hao, kwa matumaini
waliendelea kumsubiri Pinda kwa zaidi
ya dakika kumi bila mafanikio, huku viti
vilivyoandaliwa kwa ajili ya picha ya
pamoja vikiwa vimetelekezwa na
mkutano ukiendelea kama kawaida ndani
ya ukumbi huo.
Baada ya muda alijitokeza kijana ambaye
inasemekana ni mmoja wa wafanyakazi
kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira akisema kuwa; “Jamani
tuliwaalika watu wachache Waziri Mkuu
ameshamaliza na ameondoka, kama kuna
mtu hajamsikiliza Press release (taarifa ya
vyombo vya habari) ya Waziri Mkuu ipo
akatoe ‘photocopy’ karatasi ipo kwa yule
dada, (huku akionyesha mmoja kati ya
waandishi waliokuwa ndani ya ukumbi na
kwa wale wa Tv naomba mchukue kwa
kaka pale wa Tumaini.”
Akiwa mkoani Mwanza wiki iliyopita,
Pinda anadaiwa kuwaeleza wajumbe hao
wa CCM kuwa ameamua kuwania nafasi
ya Urais baada ya kushawishiwa na
viongozi wakuu wastaafu na viongozi wa
dini.

HATARI SANA: WASANII WAANDAMANA NUSU UCHI NCHINI KENYA..JIONEE MWENYEWE HAPA!

 
Siku hizi ishu ya kuvua nguo kuonyesha msisitizo au kulipigia kelele jambo flani imekua kawaida, yani wengi wameitumia hii njia kufikisha malalamiko yao na mfano mzuri ni hivi karibuni kwa Wanafunzi wa kike kwenye shule ya sekondari ya Wasichana Tabora Tanzania kubaki nusu uchi kwa nia ya kupigia kelele matatizo ya shule ikiwemo maji.

Nchi jirani ya Kenya matukio kama haya yamekua mengi pia lakini hawa ndio wamechukua headlines kwa kuwa Wanamuziki wa kwanza kuandamana kwa aina hii.

Ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich amesema Wasanii hawa waliandamana nje ya ofisi za Nation Media Nairobi wakiwa nusu uchi kulalamikia nyimbo zao kutochezwa na vyombo vya habari.

Wakiwa na mabango yao Wasanii hawa kutoka maeneo ya Vitongojini walisema wanaumizwa na kitendo cha nyimbo zao kutochezwa, wamekua wakitoa nyimbo mpya kila wakati lakini hazichezwi kwenye Radio wala TV badala yake zinazochezwa ni za wasanii walewale kila siku.



HABARI KAMILI: WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MBALIZI


Viti vikiwa vimeharibika baada ya ajali kutokea 


Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 


Eneo hili la ubavuni ndipo eneo ambalo Daladala hiyo iliingia na Kujigonga 


Gari hilo aina ya Tata likiwa limepaki pembeni Muda mchache baada ya kupata ajali hiyo


Askari wa usalama wa Barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo


Eneo ambalo Daladala hiyo iliyofumuka 





Hivi ndivyo Daladala hiyo iliyokuwa ikitoka Mwanjelwa kuja Mbalizi ilivyo  Haribika Baada ya ajali hiyo.

WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.




Ajali hiyo ilitokea leo majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV. 



Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso ilikuwa ikiingia barabarani. 


Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari. 


Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4. 


Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao. 


Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne. 


Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio.

PENZI LA MAINDA LAGOMBEWA NA WANAUME KIBAO SOMA ZAIDI HAPA

 

Staa  wa  Filamu  za  Kibongo  aliyeamua  kumpokea  Yesu, Ruth Suka  'Mainda'  amesema  amekuwa  akipata  wakati  mgumu  kumjua  mwanaume  wa  kweli  ni  yupi  ambaye  anaweza  kumuoa  na  ndoa  yake  ikawa  na  raha  badala  ya  majuto  kama  ilivyo  kwa  baadhi  ya  wasanii  wenzake....


Mainda  alisema  hakuna  kipindi  kigumu  kama  kujua  yupi  ni  mwanaume  sahihi  wa  kumuoa  na  hili  limekuwa  likiutesa  moyo  wake  japo  sasa  ameamua  kumwachia Mungu  wake  ili  amsaidie  kwani  kwa  akili  zake  ameshindwa...

"Hakuna  wakati  mgumu  kama  kipindi  cha  kumpata  mume  sahihi  kutoka  kwa  mungu, kwani  ukijichanganya  unaweza  kuchukua  mwanaume  ambaye  si  wako  na  kusababisha  kuwe  na  mafarakano  ndani  ya  ndoa  na  hili  ndio  linaumiza  kichwa  changu  kwani  mpaka  sasa  sijajua  ni  yupi  kati  ya  wengi  wanaohitaji  kunioa," alisema  Mainda

Msanii  huyo  alisema  anajifunza  mambo  mengi  kupitia  ndoa  za  watu  waliomtangulia  kwani  nyingi  zimejaa  vurugu  likiwemo  suala  la  kusalitiana  na  kuambukizana  magonjwa  ya  zinaa  kama  vile  Ukimwi  na  menginenyo, hivyo  naye  hatapenda  awe  miongoni  mwa  ndoa  hizo

TUMEAMIA HUKU