Featured Posts

Thursday, August 28, 2014

LIPUMBA ADAI RAIS KIKWETE AMEPOTEZA DIRA

Profesa Lipumba alisema Rais Jakaya Kikwete
ameshindwa kusimamia ahadi zake, hali
inayochangia kupwaya kwa utawala wake.
Akifafanua hoja yake, mwanasiasa hiyo
alisema, “Katika hotuba yake ya mwisho wa
mwaka 2011 ambapo pia alianzisha mchakato
wa Katiba, alisema kutakuwa na kituo cha
kufua umeme cha megawati 300, kutakuwa na
Kinyerezi (I) ya megawati 200, megawati
nyingine 200 za makaa ya mawe na uzalishaji
wa umeme kwa upepo.
“Hadi sasa imeshapita miezi 36, hakuna hata
kimoja alichomaliza kukitekeleza, kituo cha
kufua umeme cha Kinyerezi (I) kinaendelea
kujengwa.”
“Kwa jumla, Kikwete ameshapoteza dira ya
maendeleo kwa kipindi cha miaka tisa
alichokaa madarakani, hivyo sioni cha
kumshauri. Alisema tangu Kikwete aingie
madarakani, hakuwa na ajenda maalumu ya
maendeleo, ndiyo maana nchi imeendelea
kuwa maskini.
“Kwa sasa, Rais Kikwete amebakiza muda wa
mwaka mmoja, hakuna la kutegemea. Kwanza,
hakuwa na mtazamo au dira ya kufanikisha
mambo, kwa hiyo kwa mwaka huu mmoja
huwezi kutegemea kuwa ataleta mabadiliko
makubwa,” alisema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba, akirejea utawala wa kiongozi
wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin
Mkapa, alisema kuwa utawala wa Kikwete
umeshindwa kuwa na nidhamu ya fedha kiasi
cha kuzorotesha uchumi.
“Ili uweze kusimamia maendeleo ya nchi yetu,
ni lazima uwe na matumizi mazuri ya fedha za
umma na uwe na Serikali inayosimamia vizuri
matumizi na malengo yaliyowekwa,” alisema
msomi huyo wa nyanja ya uchumi.
“Rais Mkapa alikuwa na nidhamu ya utendaji
wa Serikali kibajeti, kwa sababu alikuwa
akitumia bajeti ya fedha taslimu. Ilitumika
kuleta nidhamu kwa kuwa fedha zilizokuwapo,
ndizo zilizotumiwa.
“Tatizo kubwa ambalo limejitokeza katika
kipindi hiki… Bajeti kwa ujumla wake, ule
mgawanyo wa kila wizara haukuwa na
mwongozo mzuri wa nini Serikali itatekeleza.
Tatizo hilo lilikuwa ni muhimu kwa awamu ya
mwanzo kuleta nidhamu katika matumizi ya
ujumla yalingane na mapato, lakini hilo jambo
limeendelea mpaka leo.”
Chanzo: Mwananchi

TUMEAMIA HUKU