Featured Posts

Friday, August 29, 2014

CHUJI ASAKWA MCHANGANI BAADA YA KUTOROKA NA SH 60000...NJAA KALI KWELI

ALIYEKUWA kiungo wa Yanga , Athuman Idd
‘ Chuji ’ inaelezwa kuwa ameingia mitini na
fedha kiasi cha shilingi 60 ,000 za timu ya
Mazombi FC ya Gongo la Mboto ambazo
alipewa kwa ajili ya kuichezea katika nusu
fainali ya Kombe la Ng’ ombe .
Mtoa taarifa kutoka kwenye timu hiyo ambaye
aligoma kutaja jina , alisema Chuji alichukua
fedha hizo kwa ajili ya kucheza katika nusu
fainali iliyopigwa Jumapili iliyopita kwenye
Uwanja wa Kampala Gongo la Mboto katika
mechi dhidi ya Waasi FC, lakini hakuonekana.
“ Baada ya kumpa hizo fedha alikubali lakini
mwisho wa siku hakutokea . Hatukubali ,
tunamfuata hukohuko kwenye mazoezi ya timu
yake ya Mwadui FC ili atupe chetu, kama
hataki si angesema tu , ” alilalama mtoa taarifa
huyo.
Gazeti hili lilipompigia Chuji simu hakupokea
na hata baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa
maandishi kuhusu suala hilo, hakujibu
chochote.

TUMEAMIA HUKU