Featured Posts

Thursday, August 28, 2014

KONDOM ZA MALAYA WA MOROGORO ZAHATARISHA.MAISHA YA WATOTO WA SHULE

Biashara ya ngono iliyokithiri katika mji
wa Morogoro imegeuka kuwa kero kwa
wakaazi wa eneo hilo na familia zao hali
inayowaweka hatarini zaidi watoto
wadogo wasio na hatia wanaokutana na
kondom zilizotumika huku mkuu wa
Mkoa huo, Mheshimiwa Joel Bendera
akinawa mikono kuhusu suala hilo.
Wakati hayo yakiendelea Morogoro,
serikali kuu imekuwa ikitafuta dawa kali
ya kuweza kudhibiti biashara hiyo hapa
nchini.
Edson Mkisi Jr wa Times Fm, hivi
karibuni alitembelea mkoa huo na
kushuhudia kushamili kwa biashara ya
ngono sehemu mbalimbali za mkoa wa
Morogoro hususani katika maeneo ya
Kaumba na Itigi mkoani humo.
Taarifa zilizopatikana awali toka kwa
baadhi ya wakazi wa maeneo ya mji wa
Morogoro zilidai kuwa biashara ya ngono
imekuwa kero mkoani humo kutokana na
utupwaji hovyo wa kondom zilizotumika
katika mitaa hiyo.
Kondom hizo zilizotumika zinahatarisha
afya ya watoto wanaozitumia kama
mapulizo.
“Kiukweli hii biashara mbali ya kutuaibisha
sisi akina mama lakini pia inatukera sana
kutokana na utupwaji hovyo wa kondom
unaofanywa na hao akina dada….na baada
ya kondom hizo kutupwa watoto wetu
wanaziokota na kuanza kupuliza kama
maputo kwakweli inatukera sio siri,”
anasema mama Sakina mfanyabiashara
maarufu wa samaki Msamvu Morogoro.
Baadae mwendesha bodabodo eneo hilo
alimuonysha mwandishi wetu Hotel moja
maaufu na kudai kwamba Hotel hiyo
imekodiwa na MALAYA hao kwa ajili ya
kufanyabiashara hiyo na serikali ya mkoa
wanatambua ‘ishu’ hiyo!
“Yaani hawa akina dada wakiwa ndani ya
hiyo Hoteli hakuna mtu anayeweza
kuwakamata ila wakifanya biashara yao nje
ndio wanakamatwa na polisi kwa huku
Morogoro maarufu kama Voda Fasta,”
anasema dereva bodaboda huyo.
Kutokana na malalamiko mengi toka kwa
wakazi wa Morogoro kuhusiana na uwepo
wa MALAYA hao katika viunga
mbalimbali vya mkoa hao, Edson Mkisi Jr,
mtangazaji wa kipindi cha Hatua Tatu cha
times fm, aliamua kuwasiliana na Mkuu
wa mkoa huo, Bw. Joel Bendara kwa ajili
ya kujua serikali ya mkoa inafanya
jitihada gani katika kupunguza ama
kumaliza kabisa kero ya MAKAHABA hao.
Mkuu huyo wa mkoa alidai kwamba
hawezi kuzungumzia suala hilo la
MAKAHABA wala utupwaji hovyo wa
kondom kwa maelezo kwamba suala hilo
lina hadhi ndogo sana ukilinganisha na
cheo chake!
“Jamani hilo suala ni dogo sana
kulingumzia mtu kama mkuu wa
mkoa….naomba ufuate protoko mimi siwezi
kuzungumzia kondom ukilinganisha na
hadhi yangu hilo suala linamuhusu Mkuu
wa Wilaya (DC), Meya ama Diwani sio mimi
jamani,” alisema Bw. Bendera.
Alipoambiwa kwamba yeye ni kama rais
wa mkoa na si vibaya kuweza kutoa neno
kuhusiana na kero hiyo Mkuu huyo wa
mkoa alisema; “Sasa hata kama ni rais wa
mkoa ndio najua kila kitu? Kwa hiyo hata
Kikwete anajua kila kitu kuhusu
Morogoro? Ebu jaribu kuwa mtafiti
kwanza hilo suala ni la level ya chini sana
kuna watu sahihi wa kuweza kuzungumzia
sio mimi…,” alisema Bendera.
Baada ya Mkuu huyo wa Morogoro
‘kumtolea mbavuni’ mwandishi wetu,
mwenyekiti wa serikali za mitaa, mtaa wa
Mwanzo Mgumu, Bw. Said Omari Kamba,
mbali ya kukiri kukithiri kwa biashara
hiyo, pia alikwenda mbali na kudai
kwamba eneo la Itigi pia ni kichaka cha
wauzaji na wanunuaji wa dawa za
kulevya.
Credit: Times Fm

TUMEAMIA HUKU