Featured Posts

Thursday, August 28, 2014

DUDE ASHINDWA KUJIUNGA BONGO MOVIE

KUTOKANA na mgogoro unaoendelea ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity, msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kwamba amekwama kujiunga na klabu hiyo japo alikuwa kwenye utaratibu huo.
Msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ akiwa ndani ya ofisi za Global.
Akistorisha na paparazi wetu, Dude alisema baada ya kuona ushirikiano waliokuwa wakionesha wanachama wa Bongo Movie kwenye misiba iliyotokea mfululizo aliamua kujiunga nao ambapo alikuwa kwenye utaratibu wa kuchukua fomu lakini kutokana na mgogoro ulioibuka hivi karibuni na katibu wa kundi hilo, William Mtitu kujiuzulu, ameamua kujiweka pembeni kwanza.
“Nilitaka kujiunga na Bongo Movie lakini nilikuwa bado sijachukua fomu ndiyo nilikuwa kwenye utaratibu huo lakini nimevunjwa nguvu na huu mgogoro unaoendelea, nimejiweka pembeni ili nisijumlishwe huko, nasubiri wakishakaa sawa nitaenda kuchukua fomu,” alisema Dude

TUMEAMIA HUKU