Featured Posts

Friday, August 29, 2014

KUMBE NUHU MZIWANDA KUJICHORA TATOO YA SHILOLE ALIWAIGA WASANII HAWA

Mwimbaji wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda
aliwashitua wengi baada ya kujichora tattoo
yenye jina la mpenzi wake ‘Shilole’, tattoo
ambayo haifutiki daima. Kitu ambacho
kiliwashitua wengi.
“Mimi nimefanya hivi kwa kupenda kwangu,
sijalazimishwa na mtu. Nimejisikia kufanya
hivi kwa sababu nampenda sana Shilole…
tukiachana basi lakini mimi nitabaki nayo hadi
nitakapoenda kaburini.” Nuh aliiambia tovuti
ya Times Fm.
Hata hivyo, Shilole alisema kuwa hatajichora
kwa kuwa Nuh kafanya hivyo na kwamba
anashukuru kwa uamuzi wake kwa kuwa
hakulazimishwa na ni ishara ya upendo wa
kweli tofauti na aliowahi kukutana nao awali.
“ Siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini
basi ni mapenzi tu na mimi siku nikiamua
kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya
yeye. Kiukweli ana love ya ukweli kabisa
tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu
walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na
ShiShi kwa kutaka kutafuta kick na lakini Nuh
kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa.
Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi.
Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu
hakuandikii barua. ”
Uamuzi wa Nuh Mziwanda unaendana na
uamuzi alioufanya Nick Cannon na Mariah
Carey mwaka 2008 walipojichora tattoo za
kudumu kwenye miili yao baada ya kufunga
ndoa. Nick aliandika mgongoni ‘Mariah’, na
Mariah alijichora kipepeo chini ya mgongo na
kuandika maandishi madogo ‘Mrs Cannon’.
“Kwangu mimi pete ni maalum na zinavutia,
lakini tattoo zinamaana zaidi kitu chochote. Ni
za milele na milele…” Alisema Mariah Carey.
Hivi sasa Mariah na Nick Cannon
wametengana na kwa mujibu wa vyanzo vya
uhakika wanasubiri talaka tu.
Lakini wamebaki na alama za tattoo kwenye
maisha yao ambazo hazitafutika daima hata
watakapokuwa na wapenzi wengine.
Hata hivyo, tattoo inaweza isiwe kitu kama
watoto wao mapacha ambapo pia ni
kiunganishi kikubwa katika maisha yao.
Je, Nuh Mziwanda na Shilole wao watafikia
hatua ipi? Je, watadumu kama tattoo ya Nuh
Mziwanda au watayeyuka na kuachiana alama
za maandishi na….!

TUMEAMIA HUKU