Featured Posts

Thursday, August 28, 2014

HUYU NDIYE MSANII BONGO MOVIE ANAYETESWA NA RUSHWA YA NGONO

Msanii wa filamu , Salma Omary ‘ Sabby’
ameamua kufunguka kuwa ameteswa sana na
rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo
pindi alipokuwa akifurukuta kutoka kisanii. Akizungumza na Ijumaa Sabby alisema, tatizo
hilo la rushwa anaweza kuwa miongoni mwa
wasanii waliosumbuliwa sana wakati kuna
baadhi walipokuwa wakitolewa nje , walikuwa
wanajenga bifu naye na wengine kumtishia
kumharibia.
“ Mimi kitu ambacho kinaniumiza sana mpaka
leo ni jinsi wanawake tunavyodhalilishwa kila
siku, naumia mno nimepita katika tabu nyingi
mpaka nafikia hapa leo , ila namshukuru
Mungu siku zote , ” alisema Sabby ambaye
ameng’ ara kwenye filamu kama vile Siri ya
Gining, Hard Price , Moto wa Radi , Dr . Ray na
nyinginezo .

TUMEAMIA HUKU