Featured Posts

Friday, August 29, 2014

DIVA NA ANTI EZEKIEL HAPATOSHI.. BIFU ZITO.. CHANZO UJAUZITO

JAMBO limezua jambo ! Staa wa sinema za
Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson amemvaa
prizenta wa Kipindi cha Ala za Roho cha Redio
Clouds FM , Lovennes Malinzi ‘ Diva’ kwa
madai kwamba amemtangaza mitandaoni
kuwa amepachikwa ujauzito na mume wa mtu
ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘ Diamond’ ,
Moses Peter ‘ Moze Iyobo’ , jambo ambalo ni
uongo . Akizungumza kwa masikitiko ya hali ya juu,
Aunt alisema kuwa hakutegemea mtu kama
Diva angetumia nafasi yake ya utangazaji
kumchafua akimsingizia kuwa ni mjamzito ,
jambo ambalo limemsababishia matatizo
kwenye ndoa yake na mumewe Sunday
Demonte.
“ Mwanamke kuwa mjamzito si jambo baya
lakini kunichafua mbele ya jamii eti nina
mimba ya Moze Iyobo, imeniuma sana .
“ Hebu vuta picha wakwe , mawifi na
mashemeji ambao tayari wameshasikia na
kusoma kwenye ukurasa wa Diva, akisema
mimi nina mimba ya yule mtoto, dah!
Nimeumia sana , kwa kweli siwezi kuliacha
lipite hivihivi . “ Huyo Diva lazima nitasimama naye
mahakamani ,” alisema Aunt.
Hivi karibuni, kwenye ukurasa wake wa
Instagram , Diva aliandika : “ Wakati sakata la
mtoto mzuri Aunt Ezekiel ana mimba ya Moze
Iyobo likipamba moto , mimba ambayo ni
tangu Mwezi wa Ramadhan , sasa hesabuni
miezi , hapa ni miezi miwili au mitatu . ”

TUMEAMIA HUKU