Featured Posts

Sunday, August 31, 2014

NOMA SANA HII MAJBAZI WAMBAKA MWALIMU KWA ZAMU MKOANI SIMIYU...SOMA ZAIDI HAPA

wanaosadikiwa kuwa majambazi
wamemteka na kumvamia mwalimu
mmoja na kumpora kiasi cha zaidi ya Sh
milioni 20 na kisha kumbaka mwalimu
mwingine wa kike katika kijiji cha Nassa
Ginery wilayani Busega mkoani Simiyu.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika mkoa
wa Simiyu, tukio hilo lilitokea usiku wa
kuamkia juzi kijijini hapo.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
mkoani Simiyu, Evance Mwijage ndiye
aliyethibitisha kuwapo kwa tukio hilo
alipozungumza na mwandishi wa habari
hizi kwa njia ya simu.
Hata hivyo, hakuwa tayari kuelezea zaidi
taarifa juu ya tukio hilo, akisema alikuwa
anasubiri jalada la Polisi kutoka wilayani
Busega ambalo lina taarifa za kina, ikiwa
ni pamoja na watu wanaohusishwa na
tukio zima.
Lakini kwa upande wa mwalimu
aliyetekwa na kuporwa fedha, Samwel
Mbochi alisema siku ya tukio, watu
anaoamini kuwa ni majambazi waliruka
ukuta wa nyumba yake na kumvamia na
kumshikilia wakimtaka atoe pesa.
Anasema alitii amri yao na kutoa kiasi
hicho cha fedha alichokuwa amekiandaa
kwa ajili ya kununua bidhaa kesho yake,
kwani pamoja na kuwa mwalimu, pia
amekuwa akijishughulisha na biashara ya
duka kijijini hapo.
Anaongeza kuwa, baada ya kuchukua
fedha, walivamia chumba kingine cha
mwalimu wa kike ambaye ni mpangaji
wake na kumbaka kwa zamu, kisha
kutokomea kusikojulikana.

TUMEAMIA HUKU