Mmoja kati ya wachezaji wa Nicki Minaj
ameng’atwa na nyoka aina ya Anaconda mwenye
urefu wa futi 6 wakati wakifanya mazoezi ya kwa
ajili ya show ya tuzo za video za MTV (MTV Video
Music Awards).
Kwa mujibu wa TMZ, Nicki Minaj alikuwa jukwaani
na dancers wake wakifanya mazoezi ya kucheza
hit ya ‘Anaconda’ ambapo dancer mmoja wa kike
aling’atwa na moja kati ya nyoka waliokuwa
wamewekwa kwenye kontena kwa ajili ya kufanyia
mazoezi. Inaelezwa kuwa nyoka hao aina ya Anaconda
hawakuwa na sumu lakini wana uwezo wa
kusambaza bacteria ambao husababisha matatizo
kiafya.
Msichana huyo alipelekwa hospitalini kupata
matibabu.
Haijulikani kama bado Nicki Minaj atapanda na
nyoka hao katika jukwaa la MTV VMAs, Jumapili .
Nicki hatakuwa mwimbaji wa kwanza kupanda na
nyoka kwenye tuzo hizo, mwaka 2001 Britney
Spears alipanda na joka kubwa wakati anaimba
‘I’m A Slave 4 U’.