Featured Posts

Friday, August 29, 2014

SAKATA.LA OKWI KUTIMUKIA SIMBA MANJI AJA JUU

BAADA ya jana uongozi wa timu ya Simba
chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ,
Zacharia Hans Pope , kutangaza kumsainisha
mshambuliaji , Emmanuel Okwi , raia wa
Uganda , uongozi wa Yanga kupitia mwenyekiti
wake, Yusuph Manji , mchana huu nao umetoa
tamko rasmi la kumshitaki mchezaji huyo kwa
shirikisho la soka nchini (TFF ) pamoja na
viongozi wa Simba na Klabu hiyo .
Katika mashitaka hayo Yanga imemshitaki
Okwi , Simba na viongozi wake kwa kuvunja
mkataba wakati mgogoro wa mchezaji huyo
na Yanga ukiwa haujapatiwa ufumbuzi . Manji
amesema katika madai hayo wanadai fidia ya
dola milioni mia tano za Kimarekani .
Wakati huohuo , kocha wa kikosi hicho Mbrazil
Marcio Maximo ameelezea kuimarika kwa
kikosi chake kwenye kambi ya wiki mbili
waliyofanya Visiwani Unguja na Pemba .

TUMEAMIA HUKU