Featured Posts

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday, June 30, 2014

UKATILI, MME AMPIGA MKE NA NYUNDO KICHWANI, AMCHARANGA KWA MAPANGA MWILI MZIMA,SOMA HAPA

DAH! Inasikitisha sana jamani. Faustina Selali, 38, mkazi wa Mgeta, Mvomero mkoani hapa, yupo kwenye mateso makali akijiuguza kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina la Lugasiani John Miasiku, kisa kikiwa ni mumewe huyo kutaka kuoa mke wa pili.
Faustina Selali,akiwa katika maumivu makali baada ya kushambuliwa na mumewe.
Mwanamke huyo amelazwa katika wodi nambi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ambapo amesimulia kisa chote mbele ya kamera ya Uwazi.
KISA CHENYEWE
Akizungumza kwa tabu, Faustina alisema tukio hilo lililobadilisha historia ya maisha yake na kumwachia machungu moyoni mwake, lilitokea Juni 25, mwaka huu majira ya saa nne usiku ndani ya nyumba yao.
“Mimi na mume wangu tumeishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 20 na kufanikiwa kupata watoto watano. Kwa kipindi kirefu nilihisi ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, wakati naendelea kumchunguza, mume wangu akaniambia anataka kuoa mke wa pili,” alisema Faustina kwa uchungu na kuongeza:
“Nikamhoji mume wangu, dini yetu hairuhusu jambo hilo na zaidi ya yote anachotafuta kwa huyo mke wa pili ni kitu gani wakati tayari mimi nimeshamzalia watoto watano na bado naendelea kuzaa?
“Hakuwa na jibu la maana, akaendelea kushikilia msimamo wake. Mwisho nikaona nisimlazimishe sana, nikamwambia kama hivyo ndivyo basi tugawane mali ili mimi niondoke aje huyo mwenzangu kwani sitakuwa tayari kuishi maisha ya uke wenza. Kwa kweli hakuwa na jibu la maana.”
Akionyesha sehemu ya jeraha.
HARUFU YA KIFO
“Ugomvi huo ulitokea Jumanne, kesho yake yaani Jumatano (siku ya tukio) mume wangu alivyorudi shamba nilimtengea ugali kama kawaida. Alikula vizuri tu... tukapanda kitandani kulala, kama unavyojua tena wanandoa muda wao wa kuzungumza kwa utulivu ni usiku, nikaamua kuutumia muda huo kumwuliza mwenzangu.
“Nikamwambia kama bado ana msimamo wake uleule, anipe sehemu yangu niondoke zangu. Hapo nikawa nimechokoza moto. Ilikuwa ghafla tu, aliamka kitandani na kuchukua nyundo kisha akaileta kichwani na kunipiga nayo, baadaye akanipiga mdomoni na kuning’oa meno mawili ya mbele kwa kutumia ile nyundo.
“Hakuishia hapo, akanitoa panga kisha akanicharanga mikono yote, palepale damu zikaruka kama kachinja ng’ombe. Nilihisi maumivu makali sana, sikuwahi kupata maumivu makali kama yale. Kusema ukweli nilichanganyikiwa kabisa na kile kipigo.”
ATUMIA UJANJA KUJIOKOA
“Wakati akiendelea kunipiga bila huruma, alikuwa akisema dawa yangu mimi ni kufa ili aweze kumchukua huyo mwanamke wake bila usumbufu. Nilivyosikia hivyo ikabidi nitumie akili; nikajiangusha chini na kujifanya nimekata kauli ili nisiendelee kuumia.
“Alipoona hivyo kweli akaniacha. Akavaa nguo zake na kukimbia. Mwanangu mdogo Nesto akanisaidia kunikongoja hadi kwa jirani yetu Mzee Chota ambaye naye aliita majirani haraka, ilikuwa ni saa sita usiku, wakanikimbiza hadi Zahanati ya Mlali lakini nikapewa rufaa ya kuletwa hapa kutokana na hali yangu kuwa mbaya.”
Kwa mujibu wa Bi. Faustina, licha ya mume wake kumfanyia ukatili huo, ndugu wanaofika hospitalini hapo kumjulia hali, wanasema mumewe bado hajakamatwa na amekuwa akiendelea kutoa vitisho dhidi yake.
Uwazi lilifunga safari hadi kijijini Mgeta kwa lengo la kuhojiana na mtuhumiwa huyo na kufanikiwa kumkuta lakini alipomuona mwandishi wetu, Miasiku alitimua mbio akidhani alifuatwa na askari.

MAJANGA, MTOTO MIAKA 6, HAKUI, HAONGEI TAFADHALI SOMA HAPA UMSAIDIE MTOTO HUYU

HUSSEIN Jumbe ni mtoto mwenye miaka 6 sasa, lakini hakui, kwani hajaweza kukaa  wala  kuongea, mwonekano wake ni sawa na mtoto wa  mwaka mmoja, imekuwa kilio  na majonzi kwa mama yake  mzazi, Rukia Twalibu, mkazi wa Kilwa –Masoko, Mkoa wa Lindi.
Mtoto Hussein Jumbe  mwenye umri wa miaka 6 sasa.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Rukia alisema alimzaa  Hussein mwaka 2008 huko Kilwa lakini katika kukua  imekuwa ni tatizo kubwa  ambalo linaambatana na kushindwa kuongea wala kukaa.
“Hapa unapomuona anasikia kila kitu, anajua kila unachomuuliza lakini  hawezi kukaa wala kuongea. Muda mrefu nampakata au  analala tu,” alisema mwanamke huyo.
Mtoto Hussein Jumbe akiwa na mama yake mzazi, Rukia Twalibu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Alisema baada ya mwanaye huyo kufikisha miaka miwili, baba yake mzazi alitoweka katika mazingira  ya kutatanisha hadi sasa  hajulikani alipo kitu ambacho  kimempa wakati mgumu sana.
Akaendelea: “Nilipobaini hali hii ya mtoto na sina msaada, nilikwenda Hospitali ya CCBRT (jijini Dar) lakini madaktari wa hospitali hiyo walisema ukubwa wa tatizo la mwanangu  hawawezi kufanya chochote.
“Juni 22, mwaka huu ndiyo nilikuja hapa Muhimbili ambapo  mwanangu anachunguzwa kisa cha kutokua kama watoto wengine ilhali umri unakwenda, bado madaktari hawajaniambia chochote, naamini wanaumiza kichwa kujua tatizo.
Bi. Rukia akijaribu kumkalisha mwanaye.
“Hadi kufika hapa Muhimbili nimepata michango kwa watu  pia nilipata barua kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi  ambayo ilinisaidia kupata kiasi  kadhaa cha pesa,” alisema mama huyo.
Rukia na mwanaye amelazwa  katika Wodi ‘A’ ya Watoto, kwa  aliyeguswa na tatizo la mtoto  Hussein, awasiliane na mama  yake kwa namba 0714 177 071.
Naamini ukimsaidia mtoto huyo, utapata baraka katika kila ukifanyacho.

MAMA WA MTOTO WA MIAKA MIWILI,ASEMA: ‘HATA MIMI NAPENDA KUISHI KAMA WENGINE’

NI kweli kama binadamu hujafa hujaumbika! Maana ya msamiati huu ni kwamba, siku binadamu anapoingia kaburini ndipo kuumbika kwake kulivyo!
Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo Kata ya Vigwaza Wilaya ya  Bagamoyo, Pwani amejikuta katika wakati mgumu kufuatia mguu wake wa kushoto kuvimba mfano wa tende kwa ugonjwa ambao bado haujapata tiba.
Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo Kata ya Vigwaza Wilaya ya  Bagamoyo, Pwani anayesumbuliwa na uvimbe mguuni.
Kwa mujibu wa mwanamke huyo mwenye mtoto wa kike wa miaka miwili, kabla mguu huo haujafika kwenye kuvimba alianza kwa kuhisi maumivu makali sana.
TATIZO LILIVYOANZA
Anasema: “Ilikuwa mwaka 2004, kilianza kitu kama kipele baadaye uvimbe wa kawaida lakini cha ajabu uvimbe huo ukawa unanisababishia maumivu makali mno mpaka kujiuliza ni kitu gani? Sikuamini kama ni uvimbe wa kawaida.
“Kadiri siku zilivyokuwa zikienda mbele ndipo uvimbe nao ulizidi kuongezeka na kufikia usawa wa kwenye mbavu zangu. Hali hii ilinitisha sana kiasi kwamba nikaanza kukosa amani na imani ya kuishi.”
TATIZO JUU YA TATIZO
“Mbali na maumivu hayo, likazuka tatizo jingine. Nikawa napata homa kali sana hasa nyakati za usiku.
“Lakini pamoja na hali hiyo sikukaa nyumbani tu, nilijitahidi kuhangaika kwa kwenda hospitali mbalimbali ikiwemo ya Tumbi (Kibaha) lakini sikupata matibabu yoyote zaidi ya vidonge ambavyo niliambiwa ni vya kutuliza maumivu lakini uvimbe uko palepale.”
...Hivi ndivyo mguu wa kushoto wa mama huyu unavyoonekana .
ANACHOOMBA
Nata anasema: “Niko kwenye wakati mgumu kama mnavyoniona, napata shida sana. Naomba nisaidiwe. Naomba wataalamu mbalimbali pamoja na wafadhili wajitokeza niweze kupata matibabu sahihi ambayo yataondoa uvimbe huu ili na mimi niweze kuishi kwa raha kama wengine.” 
BABA WA MGONJWA
Kwa upande wake baba mzazi wa Nata aliyejitambulisha kwa jina moja la Mumbi alisema kuwa, baada  ya kugundua gonjwa hilo kwa mwanaye alimpeleka hospitalini ili akapate matibabu lakini alichokibaini huko hakuna mafanikio yoyote zaidi ya mwanaye kuendelea kuteseka kila kukicha.
ALALAMIKIA MATIBABU
Mzee Mumbi alilalamikia matibabu ambayo binti yake amekuwa akiyapata  ambapo alisema si ya kuridhisha hivyo kumfanya mwanaye asipate nafuu yoyote ile zaidi ya kuendelea kuteseka.
“Kusema ule ukweli nilimehangaika sana mahospitalini lakini hakuna cha maana. Matibabu siyo mazuri, mwanangu anaendelea kuteseka tena akiwa na mtoto mdogo kama hivyo unavyomuona.
“Lakini kupitia nyie waandishi wa habari, nawaomba wasamaria wema wamsaidie binti yangu kwa hali na mali ili aweze kupata matibabu sahihi ambayo najua ni gharama kubwa,” alisema Mumbi.
KWA NINI ALIKATA TAMAA?
Baba huyo alizidi kuweka wazi kwamba, ilifika mahali aliamua kuacha kumpeleka mwanaye hospitalini.
 Aidha, alisema kuwa anashangaa kuona kila anapokwenda hospitali mwanaye anapewa vidonge tu jambo ambalo linafanya wakate tamaa.
KUTOKA KWA MHARIRI
Uwazi linafuatilia namba ya mawasiliano ya mwanamke huyo, ikishapatikana itatoa gazetini ili walioguswa wamsadie.

MISUKULE YAENDELEA KUMTESA MZEE WA UPAKO, MWENYEWE ALALAMA

MBALI na Askofu wa Kanisa la Full Gosple Bible Fellowship, Zacharia Kakobe kuteswa na misukule inayodaiwa kufufuliwa na baadhi ya makanisa ya kiroho nchini, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ (pichani) naye ameibuka na kucharukia suala hilohilo.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ akifafanua jambo.
Akizungumza na Uwazi juzi, Mzee wa Upako alisema suala la misukule linamtesa sana na kwamba anapingana na kufufuliwa kwao na baadhi ya wachungaji wa makanisa mbalimbali wanaojigamba kufufua misukule wakati si kweli na ni utapeli mtupu.
MZEE WA UPAKO ANAFUNGUKA:
“Kuna baadhi ya viongozi wa makanisa ya kioroho (bila kutaja majina)  wanadanganya  watu kuwa wanatoa misukule, si  ukweli kabisa ni uongo. Wanatafuta  namna ya kula sadaka za waumini wao kwa kuonekana wanaweza sana mambo ya kiroho,” alisema Mzee wa Upako na kuongeza:
“Hawa wachungaji wanatuchafua sana sisi tunaosimamia Neno la Mungu, wanaharibu Kanisa la Mungu kwa kudanganya waumini wao kwa sababu ya pesa tu. Hebu fikiria kuna wengine wanatoa hadi  shilingi 400,000 kwa mtu ili akubali kufanywa msukule feki na baadaye aombewe kanisani tena nimesikia wanatengenezewa hati za kifo kuonesha kuwa kweli watu hao walifariki dunia wakati si kweli, wamwogope Mungu.
Askofu wa Kanisa la Full Gosple Bible Fellowship, Zacharia Kakobe.
“Huo ni usanii ndani ya Kanisa la Mungu. Nasema naumizwa sana na wachungaji wa namna hii, nateseka sana na hili jambo. Ninayo mpaka CD za mahubiri za  baadhi ya viongozi wa makanisa wanaodanganya kuwafufua misukule lakini kwa busara siwezi kuwataja ila wanajijua kwa sababu hata dhamira zao zinawashuhudia.”
TURUDI KWA KAKOBE
Akikazia zaidi, Askofu Kakobe alisema, anayedai ana uwezo wa kufufua misukule ni muongo na kwamba atakuwa anaabudu shetani.
“Mwenye uwezo wa kufufua ni Yesu Kristo pekee na alifanya hivyo kwa sababu ya utukufu wa Mungu na si vinginevyo, si  binadamu wa kawaida ambaye amepewa upako wa Mungu anadanganya watu kuwa anao uwezo wa kumtoa  mtu ambaye alichukuliwa msukule,” alisema Askofu Kakobe huku akisisitiza kwamba mtumishi yeyote wa Mungu anaweza kufanya muujiza huo kwa utukufu wa Mungu lakini si kwa sababu ya kuonesha yeye anaweza.

WAKUBWA TU..LAANA AU TABIA?! BINTI WA KIGOGO ATUPIA PICHA ZA UC*I MTANDAONI

Imekuwa ni jambo la kawaida na pengine linalochukua sura mpya kwa sasa kutokana na watoto wa vigogo kupiga picha tata yaani za uch! na kuzitundika katika mitando kana kwamba wanajiuza.
Nadhani wadau mtakumbuka hapa nchini watoto wengi mastar mbali mbali wa kike wamekuwa na tabia hiyo ya kuanika miili yao katika mitandao haswa BBM na whatsapp kujinadi kwa wanaume,sina haja ya kuwataja majina hapa maana ni uandikwa wameshaandikwa sana ila bado kila kukicha wanaibuka wengine.
 
Sasa nchini Ghana nako mtoto wa kigogo mmoja ametundika picha zake mtandaoni na kuandika mwenye pesa ananitafute nitamtimizia kila kitu anachokitaka katika mwili wangu,hii inaonyesha hali mbaya sana kwani zaman tulijua watoto wa maskini ndio wanafanya uchafu huo ili kupata pesa ila kwasasa inaonekana watoto wa vigogo wamekuja kwa kasi sana katika swala la kujiuza mitandaoni.

KURASA ZA MWANZO NA ZA MWISHO ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULY 1,2014


.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC00563
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

siasa: Msajili wa vyama vya Siasa amzuia Mbowe kugombea tena uenyekiti CHADEMA

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini na mkutano mkuu wa chama hicho. Mutungi alisema baada ya kupitia muhtasari wa kikao cha mkutano mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi.
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi.
“Mjadala kuhusu ukomo wa uongozi ulishamalizika na haujadiliwi tena, ulishapitishwa na vikao halali vya chama, mkutano mkuu ulipitisha yale yaliyoamuliwa na vikao vya chini,” alisema Dk Slaa.
Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: “Chadema wamefanya mabadiliko bila kufuata katiba”
Alishauri waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.Alisema kama chama hicho hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haiwezi kuitambua ibara hiyo.Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye sasa si mwanachama wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa kazi.


“Ni vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba aliyeiwasilisha si mwanachama tena wa Chadema,” alisema katika barua hiyo

ALIYEKUWA AKIZUIA MAGARI YASIKANYAGE MAITI DAR NAE AGONGWA NA KUFARIKI PAPO HAPO, SOMA ZAIDI

WATU wawili wamefariki dunia jijini Dar es Salaam juzi akiwamo Emmanuel Ndahani (39) mkazi wa Kibamba, aliyegongwa na gari na kufariki dunia alipokuwa akiweka alama za matawi kuzuia gari zisikanyage maiti. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema Ndahani aligongwa na gari isiyofahamika kwa kuwa lilikimbia baada ya ajali hiyo. 
Alisema Ndahani alikuwa akitaka kuzuia magari yasiukanyage mwili wa Onesmo Yarimunda aliyefariki dunia baada ya kugongwa na basi la Prince Muro alipokuwa akivuka barabara. 

Kamanda Wambura, alisema Yarimunda (36), mkazi wa Kibaha aligongwa na basi hilo aina ya Scania, juzi, saa 3 usiku maeneo ya Kibamba. 
Maiti zimehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha. Dereva wa basi la Muro, Boniface Chuwa (36) mkazi wa Kibaha anashikiliwa na polisi.

PICHA : WANAFUNZI WA UDOMA WAGOMBANIA MABASI BAADA YA CHUO KUFUGWA






Askari polisi anayelinda usalama wa abiria na mali zao katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani akijalibu kutoa maelekezo kwa wanafunzi wa UDOM waliofika kutafuta usafiri kituoni hapo na kukuta hali ya usafiri hailidhishi kutokana na uchache wa Mabasi.


Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakigombania kulipa nauli kwa ajenti wa Basi la Urafika linalofanya safari zake kuelekea Iringa baada ya baadhi ya Vyuo kufungwa kwa pamoja na hivyo kufanya idadi ya abiria wa mikoani kuwa wengi kuliko mabasi yaliyopo.







Baadhi ya Abiria wakitafakari na mabegi yao baada ya kufika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani na kujikuta wakikosa usafiri kutokana na uchache wa mabasi ulisababishwa na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma kufungwa kwa wakati mmoja.





DODOMA imekumbwa na uhaba wa usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani kutokana na vyuo vikuu na vile vya kawada kufungwa katika kipindi kimoja hali iliyowasababishia abiria usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja 


na nauri kupanda kinyemela. Wanafunzi hao hasa wa Vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM), Mtakatifu Yohana, Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) na kile cha Biashara (CBE) ambavyo vina wanafunzi wengi vimefungwa kwa likizo ya miezi mitatu.

Wakiongea na mwandishi wa habari hizi walipokutwa wamezagaa katika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani walisema leo ni siku ya tatu tangu kuusotea usafiri huo bila mafanikio. Neema Binamu alisema kutokana na wanafunzi wa vyuo vyote kukutana kwa pamoja kusaka usafiri imekuwa shida kutokana na Idadi ndogo ya mabasi.
Hali iliyosababisha wenye magari wasiyowaaminifu kupandisha bei kinyemela mpaka kufikia 30,000 badala ya 17000 na wanapolipa kiasi hicho huandikiwa nauri ya kawaida tofauti na hapo hakuna anaesikilizwa.

‘’Kikubwa ni kwa vyombo vinavyohusika na usafirishaji vinatakiwa kujipanga mapema hasa wakati wa misimu kama hii ambayo vyuo vinafungwa ili kutuepushia usumbufu ambao hata hatujui kama tutondoka au la’’,
alisema
Kwa upande wao baadhi ya maajenti ambao hawakutaka kuandikwa majina yao walisema vipindi kama hivi ni vya neema kwao kutokana na siku za kawaida kura dagaa na sasa watakura kuku takribani wiki nzima. Nae Mmoja wa askari wa usalama barabarani aliyekuwepo kituoni hapo alisema yeye si msemaji lakini swala Nauri ya mabasi imegwanyika katika Madaraja matatu ambapo ni 23,000 lile la kwanza na 17,000 la
tatu. Na kuhusu upandishwaji nauri kiholela alisema hilo wanalo na wanawapitia abiria wanaosubili usafiri na kuwapa elimu ili wasilipe zaidi ya nauri iliyowekwa halali.

TUMEAMIA HUKU