Featured Posts

Friday, August 29, 2014

DAH HII NOMA SANA JAY DEE AJIWEKA KWA DOGODOGO... AMPA NDIGA ATANUE NAYO MJINI

OHOOO! Siku chache baada ya ndoa ya
Legendary wa Bongo Fleva , Judith Wambura
Mbibo ‘ Jide ’ na mtangazaji mahiri nchini ,
Gardner Gabriel Habash ‘ G Habash ’ kudaiwa
kuvunjika, gumzo limeibuka kufuatia kunaswa
kwa picha za Jide na kijana mmoja
(dogodogo) aliyetajwa kwa jina la Meddy
Ahmed ‘ Mtoto wa Vitoto’ , Risasi Jumamosi
linakupa kinaga ubaga .
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini , Mtoto wa
Vitoto huyo amekuwa na urafiki uliotukuka na
Jide kwa muda mrefu kabla na baada ya
mtafaruku wa ndoa ya Jide na mumewe
Gardner hivyo kudaiwa kuwa ndiyo faraja ya
mawazo ya mwanamuziki huyo hususan
kipindi hiki cha changamoto ya mgogoro wa
ndoa yake.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa ,
ukaribu wa Jide na bwa’ mdogo huyo ulipitiliza
kiasi cha watu wa karibu na staa huyo kuanza
kuhisi huenda wana uhusiano usiofaa .
“ Ukaribu wao ulipitiliza hadi kila mtu wa karibu
na Jide akautilia shaka, isitoshe kama
unavyojua, Jide si mtu wa kuweka mambo
yake hadharani. Mbaya zaidi Jide amekuwa
akimposti dogo huyo kwenye mitandao yake
ya kijamii, ” kilisema chanzo hicho.
APEWA NAFASI YA TATU
Wakati paparazi wetu akiendelea kukusanya
data kuhusiana na ishu hiyo , chanzo hicho
kilizidi kushibisha maelezo yake kwa kusema
Jide amekuwa akimwandika nambari tatu dogo
huyo kwenye mitandao ya kijamii ambapo
baadhi ya watu eti wanatafsiri kuwa , maana
yake ni kwanza mumewe (Gardner ), ya pili
yeye (Jide ) na ya tatu ni dogo huyo.
“ Dogo yuko sawa na Jide maana ukitaka
kuamini fuatilieni kwa ukaribu mtawaona tu
hata katika mitoko ya Jaydee ( Jide) . Kuna
picha kibao zipo kwenye akaunti yake, dogo
anaonekana akiwa kwenye ndinga (gari ) la Jide
ingawa dogo yuko makini kweli na suala hilo,
nafikiri wamewekeana mikakati ya kuwa wa
siri, ” kilisema chanzo hicho.
DOGODOGO SASA
Baada ya Jide kutopatikana hewani , Jumatano
iliyopita paparazi wetu alimtwangia simu Mtoto
wa Vitoto ili kumsikia anauzungumziaje
ukaribu wake na sista huyo ambapo baada ya
kusomewa mkasa mzima , dogo alikata simu
kwa madai kuwa sehemu aliyokuwa siku hiyo
haikuwa nzuri na kuahidi kumpigia paparazi
wetu baadaye lakini hakufanya hivyo hadi
kesho yake ( Alhamisi) alipopigiwa tena na
gazeti hili na kupokea .
ADAI NI MARAFIKI
Huku akiashiria sauti ya kutojiamini, dogo
huyo alisema yeye na Jide ni marafiki
wakubwa katika mazingira ya kawaida, pia ni
shabiki wake kama walivyo wengine ila ishu
ya picha mtu yeyote anaweza kupiga .
Kuhusu kuendesha gari linalodaiwa ni la Jide ,
dogo alisema hajawahi ila ameshapiga nalo
picha na mtu yeyote anaweza kufanya hivyo
kama ana uhusiano mzuri na mwanamuziki
huyo.
“ Jide ni rafiki yangu na mimi ni shabiki wake
wa kawaida. Kwa hiyo hilo siyo tatizo lakini
pia kuhusu gari mimi sijawahi kuendesha gari
la Jide lakini nimewahi kupiga nalo picha
kweli kama shabiki mwingine na hakuna
shida , ila siyo wapenzi , ni marafiki tu, ” alisema
Mtoto wa Vitoto.
ATUMA UJUMBE WA MASIHARA
Baada ya kuzungumza hayo , Mtoto wa Vitoto
alikata simu na baada ya dakika tatu alituma
ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwenye
simu ya paparazi wetu uliosomeka hivi : “ Acha
kunizingua mwana. ”
Paparazi wetu alipompigia simu kwa mara
nyingine kutaka kujua alikuwa na maana gani ,
dogo huyo hakupokea simu na hata
alipoandikiwa SMS kwamba atoe ufafanuzi
kuhusu ujumbe wake huo , hakujibu chochote
hadi gazeti hili linakwenda mitamboni .
MTOTO WA VITOTO NI NANI ?
Mtoto wa Vitoto ni kijana wa mjini tu , si
Mbongo Fleva wala si Mbongo Muvi ila
inadaiwa kwa sasa anafanya shughuli zake
mkoani Morogoro . Amewahi kuishi Magomeni,
Dar ambapo kwa sasa anadaiwa kuhamia
Kinondoni, Dar. Ana asili ya Zanzibar.

TUMEAMIA HUKU