Featured Posts

Sunday, August 31, 2014

MWIMBAJI WA TAARABU WA BONGO ANUSURIKA KUUAWA NA AL SHABAAB HUKO MOMBASA

Oooh nooo ! Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la
Mashauzi Classic , Aisha Ramadhani ‘ Isha
Mashauzi’ , amejikuta kwenye wakati mgumu
baada ya kuvamiwa na kundi linalojiita Al -
Shaabab ( siyo wale orijino wanaosifika kwa
ugaidi ).
Mwimbaji na Kiongozi wa Kundi la Mashauzi
Classic , Aisha Ramadhani ‘ Isha Mashauzi ’ .
Tukio hilo ambalo liliibua sintofahamu kwa
wananchi , lilitokea juzikati katika hoteli
inayojulikana kwa jina la Grassovila iliyopo
Mombasa nchini Kenya ambapo walimuibia
msanii huyo kila kitu alichokuwa nacho .
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Isha
alisema kuwa alikwenda Mombasa kwa ajili ya
mwaliko wa mashabiki wa Timu ya Arsenal ya
England waishio Mombasa na alipokuwa
akijiandaa hotelini, ghafla alishtukia watu
waliojificha nyuso wakiingia katika chumba
alichokuwepo kisha kumuamuru atoe kila kitu.
“ Nilishtuka sana kuona kundi la watu likivamia
chumbani kwangu , nasikia walianzia katika
vyumba vingine , jamaa walinichukulia kila kitu
nilichokuwa nacho hadi hati ya kusafiria lakini
namshukuru Mungu Watanzania wenzangu
walinisaidia na kuweza kurejea Bongo,”
alisema Isha .
Alisema polisi nchini humo wanaendelea
kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuwatia hatiani
‘ wahuni’ hao.
Hadi Isha anafanikiwa kurudi Bongo, hakuna
mtu yeyote ambaye alikamatwa kuhusiana na
tukio hilo.

TUMEAMIA HUKU