Natamani kama siku zingerudi nyuma na natamani nisingemjua Baba Mkwe wangu kabisa maishani mwangu.Huyu mwanaume ndio amehariba maisha yangu kabisa....
Najua wengi wenu mnaweza makaniona mimi kama shetani na mtu asiye na moyo wa kupenda na wa huruma. Ila ukweli ni kwamba mume wangu kwa moyo wangu wote, lakini tangu nianze kutembea na baba yake, naona mume wangu ahniridhishi kabisa...
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 25 na nimeolewa na mwanaume mwenye elimu ya juu sana na mume wangu ana miaka 28 na baba mkwe wangu ana miaka 55. Nina mlaumu sana mume wangu kwa sababu yeye ndiye chanzo cha hayo mambo yote kutokea maishani mwangu, yaani ya mimi kutembea na baba yake mzazi( ba mkwe wangu).
Kwa sababu mume wangu alikuwa akirudi nyumbani amelewa sana, wakati tunaanza uchumba alikuwa hana hii tabia kabisa lakini tangu tumefunga ndoa, amekuwa anarudi nyumbani akiwa amelewa sana na ni usiku sana.
Mtu pekee wa kumweleza matatizo yang alikuwa ni Baba mkwe. SIku moja mme wangu hakurudi nyumbani kabisa na niliamua kumwita baba mkwe wangu akaniambia yupo njiani anakaribia kurudi.
Alipofika nikamuelezea matatizo yangu yote na mume wangu mpaka yale yanahusu chumbani, sielewi nini kilitokea nilijikuta naanza kulia nikaelekea chumbani nikamuacha yeye yupo sebuleni. Alinufuata chumbani na kuanza kunibembeleza na kunikumbatia mpaka nikajikuta yupo juu yangu na tukajikuta tunafanya mapenzi.
Tokea siku hiyo kila siku nimejikuta nafanya nae mapenzi na natamani kumuona, naombeni ushauri wenu nifanyeje ili niliondokane na ili janga jamani...