Featured Posts

Friday, August 22, 2014

ANTI EZEKIEL AFUNGUKA NA KUDAI WEMA SIO MTOTO MDOGO WA KUFUNDISHWA JINSI YA KUISHI.. AMPA MAKAVU DIAMOND

Aunt Ezekiel ambaye ni rafiki wa karibu wa Wema
Sepetu, amejibu kauli ya Diamond Platinumz kuwa
Wema ana marafiki wanaomfundisha tabia mbaya
na kwamba kama anataka kuendelea aachane nao.
Akiongea na Bongo5, Aunt Ezekiele ameeleza kuwa
anachofahamu Diamond aliongea kwa niaba ya
watu walio karibu nae na hakumtaja yeye kwa jina.
Lakini hata kama angemtaja yeye hadhani kama
Wema ni mtu wa kufundishwa.
“Wema ni mtu mzima anaishi mwenyewe na ana
maisha yake sidhani kama ni mtu wa kufundishwa.
Wema ni mtu ambaye ana maamuzi yake, watu
hawajui kuna wakati wa kazi na kuna wakati wa
kuspend maisha. Kwahiyo mimi na muda wangu
wa kazi na nina muda wangu wakuspend.”
Amesema.
Aunt Ezekiel hajali kinachosemwa na watu kuhusu
ukaribu wake na Wema na kinachoendelea katika
kazi zake.
“Sihitaji kuangalia kuna mtu anafuatilia maisha
yangu kwamba eti nakuwaga na Wema.
Hawanisaidii chochote. Nachotakiwa kuangalia
nafanya kazi zangu na maisha yangu yanaenda
mbele na sitaangalia watu wanasema nini. Mimi
nina kazi zangu. Sijui kama Wema kama
anahitajika kubadilika kwa sababu Diamond ndiyo
anajua mapungufu ya Wema na Wema anajua ya
Diamond.” Chanzo: Bongo5

TUMEAMIA HUKU