Featured Posts

Sunday, June 8, 2014

ZIJUE ALAMA MUHIMU ZINAZOAHSIRIA HATARI KATIKA PENZI LAKO

Binadamu wanayo mabadiliko ya kiasili, hasa tunapozungumzia matendo yao, uaminifu na majaribu. Ni wadanganyifu na hupenda kuficha tabia zao nyuma ya sababu za uongo na kweli. Wakati wanawake hulaumu kwamba vitendo vya wanaume havitabiriki, lakini bado upo ukweli kuwa jinsia ya kike hujiona sahihi. Wao hudhani wanatabirika. Hata hivyo, unachotakiwa kuaamini ni hiki, A na B yote ni sawa.

Wanaume wanatabirika na wanawake ni kinyume chake. Asili ya wanaume ni kuwa wanapotoka, hukumbuka nyumbani. Kawaida yao ni kama msemo: “Mwenda tezi na omo marejeo ngamani.” Mwanaume akipata kitu ‘comfotabo’ cha pembeni ni nadra kumsahau ‘mamsapu’ nyumnbani. Hawadharau dafu, wanaamini embe ni tunda la msimu. Kinyume chake ni kuwa mwanamke akionjeshwa ‘asali ya nje’ huchonga mzinga.
Tunakaa meza moja na watu mbalimbali wenye matatizo kwenye uhusiano. Tunawashauri nini cha kuzingatia, wanayafanyia kazi yale ambayo tunawapa na kunyookewa. Hilo linakuja na tafsiri kwamba tunawajua watu wengi na kasoro zao kimapenzi.
Udhaifu mkubwa wa wanawake ni huu, hawajui kutofautisha maziwa na tui la nazi. Wanahadaika kwa weupe na kudhani A na B ni sawa. Hiyo ndiyo sababu ya kumuona ‘mista’ wake hafai na kujisajili kwa ‘Kiserengeti boy’.
Ni rahisi kumbaini kama ameanza kuchepuka kwenye njia za panya, kwani akipewa tamu nje, hurudi nyumbani na gunia la dharau na matusi kwa mume wake. Akiombwa unyumba kila siku atatoa visingizio.
Ataanza kumzingatia zaidi yule anayemtosheleza katika matamanio ya mwili na mume wake atampa ‘kadi nyekundu’. Ikiwa mzee ndani maisha yake ni pangu pakavu tia mchuzi, kisha apate kibopa anayeweza kumpa pesa ya ‘shopping’ Sabasaba, ujue wa zamani lazima atapewa kibuti. Kinyume chake ni kuwa hauwezi kusikia mwanaume anamuacha mpenzi wake kwa sababu hawezi kutoa mahanjumati kitandani au maisha ni magumu.
Hata hivyo, lengo kuu ni kutaka kujua alama za hatari kwa mpenzi wako, yaani ukizisoma kwake, basi utatakiwa ujiandae kupewa ‘red card’. 

MUDA WOTE YUKO MBALI

Ukimuomba ‘appointment’ haishiwi sababu, mara oh! Nyumbani kuna hili na lile au anakuahidi atakuja lakini mwisho wa siku hatimizi ahadi. Anasingizia ana kazi nyingi kusudi asionane na wewe. Hiyo ni alama ya hatari, ujue siku si nyingi atakuacha solemba. Wengine wameumbwa na aibu, kumtamkia mtu sikutaki ni kazi kubwa, hivyo huamua kujiweka mbali ili ujiulize mwenyewe kichwani na kupata jibu kuwa tayari ndege amekwisha choropoka tunduni.
Kama ni mume, ugomvi kidogo anaondoka na harudi mpaka kesho yake, au mke ndani ukimtibua anafungasha virago vyake na kurudi kwao ama kuweka hifadhi kwa marafiki zake, hiyo ni ishara kuwa hataki kuwa karibu na wewe, hivyo hakutaki. 

HATAKI KUFANYA MAPENZI
 
Kila mtu hufurahia mapenzi na yule anayempenda kutoka moyoni, labda awe amechoka. Lakini inapotokea mara kwa mara kila unapoomba anakupa sababu tofauti za kukutolea nje, hiyo ni alama kuwa amekuchoka.
Mapenzi ni tendo la moyoni, linalotambaa mwilini kwa hisia, hivyo lipo kisaikolojia zaidi. Pointi hiyo ndiyo inayotoa ukweli kuwa kama hataki kufanya mapenzi na wewe, maana yake moyoni mwake haumo.

ANAKUWA MPINZANI 
Wakati mnatongozana alikuwa anakusifia kwa kila kitu. Ulipovaa alikuambia umependeza, alikupongeza kuwa sura na umbo lako ni ‘matata ile mbaya’. Mlipokutana kwenye sekta ‘chumbani zaidi’, huko pia alikumwagia sifa kemkemu.
Tofauti na wakati huo, hivi sasa kila unachokifanya kinakuwa ni kibaya kwake, ukimpigia simu anakuambia umpe nafasi ya kufanya kazi, yupo ‘bize’. Ukivaa, anasema mavazi yako hayafai kuongozana naye.
Hata siku moja, mpenzi hawezi kuwa mpinzani, kama kuna mambo hayaendi sawa, basi atapigana kukubadilisha ili uende sawa na yeye, lakini kama anakuponda bila kukupa ushauri, hiyo ni alama ya hatari kwako. Mkiwa katika maongezi yenu wawili au yanayojumuisha baadhi ya marafiki, hataki kuwa upande wako. Anaweza kumsifia mtu mwingine kuwa ni mzuri kuliko wewe, hilo unatakiwa kulisoma na kushika njia mapema. 

ANAANZISHA UHUSIANO NA MTU MWINGINE
Akufukuzae hakwambii toka, vitendo vyake vitakuonesha tu! Hivi kama mtu anakupenda kwa dhati, anawezaje kuanzisha uhusiano na mtu mwingine? Jibu ni kwamba hawezi, kwahiyo ni busara uwe unasoma alama za nyakati ili maji yanapofika shingoni uwe umeshapata njia ya kukutoa kimasomaso. 

ANASEMA HATAKI KUKUONA

Baada ya kukufanyia vituko vya kila aina, sasa ameamua kukuweka wazi kuwa hataki kukuona kabisa, sasa unangoja nini kwake? Hautakiwi kuwa mtumwa wa mapenzi, mpende akupendaye, asiyekupenda achana naye.

TUMEAMIA HUKU