Featured Posts

Saturday, June 28, 2014

MAKUBWA:BINTI WA MIAKA 16 AELEZEA MAMBO MZITO KUHUSU FREEMASON

Binti Fauzia akiwa amepozi nyumbani kwao maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam.

Binti mmoja aliyetambulishwa kwa jina la  Fauzia (jina la mbele lipo), mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Kigogo jijini Dar amedai kutumikia nafasi ya umalkia katika imani yenye utata duniani ya Freemason, Uwazi linakudondoshea.

Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba ili kujiunga na imani hiyo, alimuua mama yake mdogo kwa ajili ya kafara.

 Akizungumza na gazeti hili siku chache baada ya kuokoka akiwa nyumbani kwa baba yake mdogo, Kigogo, Fauzia alisema alitokea Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akiishi na bibi yake.
 Alikuja Dar kwa lengo la kuendeleza mauaji ya kafara ambapo safari hii ilikuwa amuue mama yake mdogo mwingine ambaye ni mjamzito kwa sasa.
 Alisema kama angefanikiwa kumuua, angepandishwa cheo na kuwa malkia kamili katika jamii hiyo inayotafsiriwa vibaya duniani.
 ALIKOTOKEA
Fauzia alisema kuwa mara ya kwanza hakujua kama amekuwa mwanachama wa Freemason bali alichojua yeye alijiunga na uchawi wenye ushirika wa Kahama na Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo mara kwa mara alikuwa akija Dar usiku na kufanya mambo ya kichawi kwa watu mbalimbali.
 Alisema siku moja aliambiwa lazima amtoe uhai mama yake mdogo, naye kwa uwezo aliokuwa nao alifanya hivyo, mama yake mdogo akafa kwa kuugua ghafla.
 Baada ya kifo cha mama yake mdogo, ndipo usiku mmoja bibi kizee mmoja (alimtaja jina) alimtokea katika ulimwengu wa kiroho na kumwambia alitakiwa aende kwenye Jiji la Lagos nchini Nigeria kwa ajili ya kutambulishwa rasmi na kupewa umalkia mdogo.

Baadhi ya vitu vinavyotumika kwa ajili ya kafara.

TUMEAMIA HUKU