Featured Posts

Sunday, June 29, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AANGUKIA PUA TENA,DAVIDO ACHUKUA TUZO, BAADA YA KUTOFANIKIWA KUPATA TUZO YA BET DIAMOND ASEMA HAYA!!!


 Taarifa Mpya Ni Kuwa Tuzo Zimefanyika Na Tuzo Aliyowania Diamond Ya Best Africa Act Imekwenda Kwa Msanii Mwenzake Davido Kutoka Nigeria.

Kwenye instagram Ya Diamond Kuna Huu Ujumbe kuhusu Matokeo Hayo.

” Tusipopenda kukubali Matokeo na Ushindi wa Wenzetu basi Daima Hatutaweza kuwa Washindani….Muhimu ni kujua wapi tulipotoka na Wapi tulipo Leo… 

Katika Nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya Million 40, kuchaguliwa Tanzania ni fursa, Heshima na Hatua kubwa… Cha Muhimu ni kuitumia vyema Fursa Hii na Kuhakikisha Mwakani tunapiga Hatua Zaidi!….

 Asante sana kwa wote wanaozidi kuni support kwa hali na Mali, Mapambano ndio kwaaaanza yanaanza sasa…..!!!!!! @wcb_wasafi For Life Baby
d

dd 7


Msanii wa Nigeria, Davido ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Best African Act, katika BET Awards 2014 zinazofanyika usiku huu Los Angeles, Marekani.

DAVIDO ASHINDA TUZO
Davido alikuwa anawania kipengele hicho na wakali wengine kutoka Afrika akiwemo Diamond Platinumz, Mafikizolo, Toofan, Sarkodie na Tiwa Savage.
Na Davido ameandika Hivi Twitter Instagram

dd 4

Show kamili ya tuzo hizo imeanza muda mfupi baada ya kutoa tuzo hiyo kwa msanii wa Afrika.
Ingawa Diamond Platinumz hakubahatika kuichukua tuzo hii, lakini hatua aliyopiga ni kubwa sana inayoweka Tanzania kwenye historia ya tuzo hizo kubwa za muziki duniani.

Kabla ya tuzo hizo, Diamond alipata nafasi ya kufanya mahojiano na vituo vikubwa na kuhudhuria mkutano maalumu wa wanamuziki wa kimataifa, na jana usiku aliungana na wanamuziki wenzake wa kimataifa katika BET Pre Awards Party.

TUMEAMIA HUKU