Featured Posts

Saturday, June 28, 2014

LULU: SINA MPANGO WA KUMBEMBELEZA MWANAUME COZ WANANITONGOZA KWA SIKU WENGI SANA HATA KUWAHESABU NASHINDWA



Wakati wanawake wengine wakionekana kubembeleza penzi na kujinyenyekeza kwa wapenzi wao ili wasiachike, Lulu Michael anasema hana muda huo kwani uzuri wake unatosha kuwavuta wanaume wa kila aina kutoka katika kila kona ya Tanzania.....


Lulu amedai kuwa inawezekana mwanaume wa kwanza kwake ndo chaguo lake namba moja, lakini suala la kuanza kulilia mapenzi au kuumia halipo na kamwe hawezi kufanya hivyo. 



"Mapenzi ni magumu hasa kwetu sisi wasanii. Kuna wanaume wanaweza kuja kwako ukadhani ni wema lakini baada ya kumaliza haja zao huwaoni, ndo maana huwa sioni haja ya kujilizaliza kwa mwanaume coz akigundua umezimika ndo kabisa atakugeuza Toilet paper ya kuchambia...... 



"Najua wapo wengi sana wanaonitamani, lakini kwa taarifa yao ni kwamba nipo makini sana na naitambua thamani yangu." Alisema Lulu. 



Hata hivyo Lulu alisema kuwa huwa anatongozwa na wanaume wengi sana kutokana na uzuri alionao, hali inayomfanya abadili namba ya simu kila mara kukwepa usumbufu.

TUMEAMIA HUKU