Featured Posts

Monday, June 30, 2014

DIDA WA TIMES FM ADAI TALAKA , NDOA YANUKIA KUVUNJIKA NI BAADA YA KUMFUMANIA MUMEWE NA DOGODOGO

KIMENUKA! Siku chache kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuanza, ndoa ya Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe anayepiga mzigo TV1, Ezden Jumanne inadaiwa kuvunjika, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa kuiripoti.
Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ na mumewe,Ezden Jumanne anayepiga mzigo TV1 wakati wa harusi yao.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kililinyaka tukio zima nyumbani kwa mtangazaji huyo Mwananyamala-Manjunju, Dar, ishu hiyo ilijiri wiki iliyopita usiku ambapo majirani walimsikia Dida akilia lakini wakashindwa kutoa msaada kutokana na geti kufungwa.
Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne wakisikiliza mawaidha ya Bi. Hindu wakati wa Harusi yao.
“Tuligonga sana mlango lakini hakuna chochote ila baada ya muda tulimuona mume wa Dida akitoka nje na begi kisha akaingia kwenye Bajaj  na kuondoka, tukagundua walikuwa kwenye ugomvi,” kilisema chanzo hicho.
TATIZO NI NINI?
Chanzo kingine makini kimepenyeza madai kuwa ugomvi wa wawili hao uliibuka mara baada ya Ezden kuhoji juu ya mapato ya mkewe.
“Jamaa alikuwa anahoji mshahara na fedha ambazo mkewe anazipata katika shughuli za u-MC, alihoji pia kuhusu mwanaye kusoma Shule ya Saint Kayumba (hali ya chini) ndipo mtiti ulipoanzia,” kilisema chanzo hicho.
Bw. Ezden Jumanne akipozi.
EZDEN AENDEWA HEWANI
Baada ya kunyetishiwa ishu nzima, mwanahabari wetu, alimtafuta Ezden kwa njia ya simu na kumsomea madai hayo ambapo hakuwa tayari kufafanua zaidi, alijibu kwa kifupi:
“Elewa tu kwamba tupo kwenye matatizo na mke wangu ila kwa sasa siko tayari kulizungumzia.”

DIDA ANASEMAJE?
Kama ilivyo ada ili kupata uzani wa habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Dida, alipopatikana, alifunguka:
“Mimi na mume wangu huwa hatuna mipaka katika simu zetu, kila mtu yuko huru kuchezea simu ya mwenziye. Siku ya tukio jamaa (Ezden) kabla hajaenda kuoga alitengeneza namba za siri (pasword) sasa nilivyotaka kucheza gemu nikamfuata bafuni na kumuuliza mbona simu imefungwa, nikamuomba anifungulie, huwezi amini akaanza kunitukana, nikajiuliza ni simu tu au kuna mengine!”
Khadija Shaibu ‘Dida’.
KIPIGO KINAENDELEA
Akiendelea kusimulia, Dida alisema ghafla, Ezden alichukua mkanda na kuanza kumpiga.
“Nilishangaa sana, nikajiuliza kosa langu ni nini? Alinipiga hadi akanipasua sehemu ya kichwa, sikuamini kama Ezden anaweza kunifanya vile au kama alinichoka angeniambia wakati yeye ndiye mkosaji,” alisema Dida.
EZDEN ATIMKA
Chanzo kilidai kuwa, baada ya Ezden kuona amemuumiza mkewe, alikusanya nguo zake na kukimbia kwa usafiri wa Bajaj kwani Dida alificha funguo zote za magari yake.
“Alijua Dida atakwenda polisi hivyo akaona bora atimke zake,”  kilisema chanzo.
Khadija Shaibu ‘Dida’ na mume wake, Ezden Jumanne wakiwa nyumbani.
DIDA ATAKA TALAKA
Katika kuonyesha kuwa amechukizwa na tukio hilo la kupigwa ambalo amedai limekuwa likitokea mara kwa mara pamoja na kukosa imani naye katika masuala ya kuchepuka, Dida amesema kwa kuwa alishindwa kumuomba msamaha siku ileile ya tukio, anachotaka kutoka kwake ni talaka tu.
TUJIKUMBUSHE
Tukio la kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyofungwa mwaka jana (siku tano kabla ya Mwezi wa Ramadhani kuanza) likikamilika kwa talaka, Dida atakuwa ametimiza idadi ya ndoa tatu kuvunjika.
Awali aliolewa na Mohamed Mchopanga ‘Mchops’ kisha Gervas Mbwiga ‘G’ na wote walimmwaga kwa talaka

TUMEAMIA HUKU