Featured Posts

Sunday, June 29, 2014

BOKO HARAM WAANZA KUADHIBIWA KICHAWI......NYOKA WA AJABU NA NYUKI WAWATOA MSITUNI


Wanajeshi wa Boko Haram wanaofanya mashambulizi na kuua raia wasio na hatia huko Nigeria wamedaiwa kuanza kukimbia msitu baada ya nyoka wenye sumu kali na nyuki kuwashambulia.

Habari hizi zilielezwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na kuthibitisha kuwa ni mmoja wa member wa kundi la Boko Haram na alieleza kuwa hivi sasa kundi hilo limelazimika kuhama msitu na linaelekea maeneo ya mpaka wa Nigeria na Cameroon baada ya wanajeshi wake wa ngazi za juu kushambuliwa na nyoka na kupoteza maisha.

Kumezuka hisia za kiimani kuwa Boko Haram wanaadhibiwa na mizimu ya watu  waliowauwa kinyama. 

Jeshi la Nigeria limeshafanya juhudi za kuwaondoa msituni lakini imeshindikana  na hadi sasa kundi hilo linawashikilia wasichana zaidi ya 260 na bado linaendelea kushambulia Nigeria kwa mabomu ya kutegwa.

TUMEAMIA HUKU