Featured Posts

Friday, June 27, 2014

SHUHUDIA UNYAMA HUU INASIKITISHA SANA DENTI WA RUCO KISA CHA KUCHOMWA MOTO , TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA INAYOONEKANA KWENYE VIDOKEZO
Mwanafunzi ambaye amefahamika kwa jina moja la LEMA Alikua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO).
Taarifa  za awali zilizotufikia zimeeleza kuwamnamo tarehe 24.06.2014 mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5 Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na Binti ambaye alianza kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi. Na kwakua eneo hilo mkulikuwa na mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.

Baada ya tukio hilo wakatokea watu  (2) waliojitambulisha kuwani askari wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe kwa madai ya kumfikisha kituoni.

Lakini baada ya mwendo mfupi kuelekea kituoni wananchi wenye hasira kali walimchukua kijana huyo kinguvu na kwenda kumchoma moto.

Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa katika wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

TUMEAMIA HUKU