Featured Posts

Monday, June 9, 2014

HAPINESS MAGESE AFUNGUKA JINSI KIFO CHA KANUMBA KILIVYOKWAMISHA MIPANGO YAKE YA KUWA STAA WA BONGO MOVIE


Miss Tanzania 2001 na mwanamitindo wa kimataifa Millen Magese  amekumbuka  kauli  ya  kwamba  mipango  si  matumizi, kutokana  na  kuwa  na  mipango  mingi  na  marehemu Steven Kanumba  enzi  za  uhai  wake  katika  kuikomboa  sanaa  ya  filamu  nchini Tanzania, lakini  kabla  hawajakutana  naye  mauti  yalimkuta...
Millen  na  muigizaji  maarufu  nchini  Nigeria, Ramsey Noah  walipanga  kukutana  na  Kanumba  lakini  kabla  siku  hiyo  haijafika  kifo  kilimkuta  Kanumba  na  mipango  yote  ikaharibika....
Millen

Millen  alifafanua  hayo  katika  mahojiano  maalumu  wakati  akitangaza  kampeni  yake  ya  kuhamasisha  wanawake  wanaosumbuliwa  na  maumivu  ya  tumbo  yasiyo  ya  kawaida  pindi  wanapokuwa  katika  mzunguko  wa  hedhi  zao  ambapo  kitaalam  hujulikana  kama Endometriosis  ambapo  amegundua  kwamba  kati  ya  wanawake  100  wa  Tanzania, wanawake  12  hadi  15  wanasumbuliwa  na  tatizo  hilo...
Star wa Nigeria Ramsey Nouh na marehemu Steven Kanumba
Akikumbuka  siku  ya  kifo  cha  Kanumba  kabla  hawajakutana  na  kuzungumzia  masuala  mbalimbali  kuhusiana  na  filamu  za  Tanzania  na  namna  ya  kupiga  hatua  nyingine  mbele,Millen  alisema:

"Iliniuma  sana  kipindi  kile  maana  nilikuwa  nipo  nchini  na  tulipanga  mimi, Kanumba  na Ramsey  Noah  lakini  ndio  ikawa  hivyo  lakini  kwa  filamu  zetu  bado  tunatakiwa  kusoma  zaidi  ili  tujue  mambo  mengi  na  pia  tutengeneze  wigo  mpana  wa  marafiki  kutoka  nje  kama  mimi  kwa  sasa  nina  marafiki  wengi  akiwemo  Ramsey  Noah, Genevieve Nnaji, Albal  na  wengine  wa  Marekani"
Katika  kusaidia  tasnia  hiyo, mrembo  huyo  anayemhusudu  mrembo  na  mwanamitindo    Tausi  Likokola,Iman,Flaviana Matata, na  Harieth  Paul  alisema  mwelekeo  wake  baada  ya  kukamilisha  masomo  yake  ya  uigizaji, ataandaa  filamu  yake  binafsi  itakayoelezea  maisha  yake   halisi  na  tatizo  linalomkabili  na  pia  ataandika  hadithi  kuhusiana  na  mauaji  ya  watu  wenye  ulemavu  wa  ngozi, Albino.

"Kwa  sasa  nasomea  namna  ya  kuongoza  filamu  katika  chuo  cha  New  York  Film  Academy  nchini  Marekani, nikimaliza  nitaingia  kwenye  filamu  na  kuleta  mabadiliko  katika  uandishi  wa  hadithi  za  filamu  hizo  tofauti  na  filamu  nyingi  za  hapa  nchini  ambazo  nyingi  hutambua  zinavyoishia  baada  ya kuitazama  mwanzo  hivyo  kupoteza  ladha  ya  kuitazama," alisema  Millen  na  kuongeza:
Millen
"Movies  zetu  za  hapa  Tanzania  zinakosa  watunzi  wazuri  wa  hadithi  maana  nyingi  zikianza    unajua  zitakapoishia,hivyo  tunatakiwa  tujuane  na  wasanii  mbalimbali  kutoka  nchi mbalimbali  kama  ninavyowafahamu  baadhi  yao  kutoka  nchini  Nigeria  na  baadhi  ya  wasanii  wakubwa  nchini  Marekani  ndipo  filamu  zetu  zitafika mbali," anasema  Millen.


Pia  model huyo wa kimataifa chini ya Ford Models New York alifafanua  sababu  inayomfanya  asishuke  katika  tasnia  ya  urembo  akidai  inatokana  na  kujituma  kwake, kujifunza  zaidi  na  kutoridhika   na mafanikio  aliyoyapata  huku  akiongeza  kwamba  anaishi  na  kuwaheshimu   vizuri  wanaomuongoza  pamoja  na  watu  wote  wanaomzunguka  hasa  nchi  yake.

TUMEAMIA HUKU