Featured Posts

Friday, June 6, 2014

DUUH WABONGO WACHUKUA UMAARUFU KUPITITA DIAMOND, WAJAZANA INSTAGRAM NA FACEBOOK ZA BET

Hii sasa ni shida!!! Huenda wafanyakazi wa kituo cha BET, kama hawatakuwa wanajichekea tu kwa jinsi wabongo walivyo na fujo kwenye 
ukurasa wao wa Facebook na Instagram, basi watakuwa wanajuta kumtaja kwenye tuzo hizo.Katika utaratibu wake wa kuweka picha za nominees mbalimbali wa tuzo hizo kupitia
mitandao ya Instagram na Facebook, BET wamejikuta wakishangaa na namna ambavyo jina la Diamond limekuwa likitajwa katika asilimia kubwa ya comments hata kwenye picha zisizomhusu staa huyo wa Tanzania.
Hiyo ni kutokana na kampeni iliyoanzishwa na mashabiki wa muimbaji huyo wanaoitaka BET ifahamu nguvu yake. Kwa wengine comments hizo zimeanza 
kuwa kero kwenye ukurasa huo japo BET wanaweza kufurahia jambo moja kubwa – wamepata followers wengi kutoka Tanzania.
Pamoja na kwamba comments hizo zinaweza zisiwe na mchango wowote wa kumfanya ashinde, kituo hicho cha BET kinapata ujumbe muhimu kuhusiana na kukubalika kwake Afrika Mashariki. Ujumbe huo unaweza kuwa mwanzo 
mwingine wa Diamond kupata airtime kwenye kituo hicho kwa video zake zinazokuja hasa ya wimbo aliomshirikisha Iyanya ambayo video yake ilifanyika nchini Uingereza mwezi uliopita.
Ujumbe mwingine jumuiya ya muziki wa kimataifa inaoupata kupitia mashambulizi hayo ya mashabiki wa Diamond, ni ukubwa na ushawishi alionao hitmaker huyo wa My Number 1.
Haya ni baadhi ya maoni ya wabongo kwenye picha za Instagram za mastaa wengine yanayomhusu Diamond.
jandareal
Yupo kwenye best actor pia? Bet watakuwa wanajichekea tu
twissyben
Wabongo nomaaa kila sehemu ni sisi,,,wataisoma D’s tym iwe movie ,music ni #diamondplatnumz
nico_agust
@twissyben shida tupu!! hapa lazma watuone kuwa tuna uelewa mdogo wa mambo haya!!
jusseee
Hahhah siwanesema akuna kura bat mtu akiongelewa Sana ila sisi noma
ata kwa washereheshaji atujali no daimondplatnomz tu ata kwenye movie ivyo ivyo kweli watatupa tu tuzo na kutujua atujielewi. Unazani uwongo kweli wataangalia kahistoria ketu watatupa tu tuzo ole wao wachakachue tunamtuma kikwete nikuandamana mwanza mwisho kwa hali hii kila kit BMT ni diamond tu watunyime tuzo sasa waone
salmaasaidy
Hahahahahahaha nyamani mi nacheka sana kila post @diamondplatnumz .nimecheka kweli @jusseee
janeelingerie
Hahahaaaaaa uuuuwiii nacheka balaa daaahh kweli watu hawaelewi daaahh ila @diamondplatnumz uko juu hata hawa jamaa wataashangaa @wemasepetu
berthamagodi
Kashapata umaarufu jamaa mana kila mtu atataka amjue mana kachafua mbaya wabongo tumetisha aiseee
jandareal
Dah lkn licha ya kupata umaarufu pia itaonyesha ni kiasi gan wabongo tunaakili nzito. Aliyetoa instruction kufanya haya alikosea sana, sema bado tunahitaji elimu juu ya hili,jishtukien had movie mnacoment diamondplatnumz @diamondplatnumz tolea ufafanuzi wa hili
berthamagodi
Shida tunakurupuka hao wahusika walito bio tuingie kupiga kura kumbe kituo cha redio pia kule diom kashine mbaya sasa uku ndo kafunga kaz marekan nzima watakua wanashangaaa. Bongo noma sana
rehemaessy
Wapenzi wa dai kuweni waelewa jazeni ktk picha ya dai sio kila picha mnatuzalilisha wabongo inaonekana hatujui kusoma @desmondmshana @thatgud_girl_g @mnayanda waelewesheni na wenzenu
telhom
Guys nendeni kwa picha ya Diamond ndo mukaandike jina lake la hasha
 mkiandika hapa nikujisumbua hii si picha yake so hawatoihesabu please go back to @betawards then chagua jina la @diamondplatnumz ndo uandike jina lake mbona mko wagumu kuelewa jamani
nakupendapia
Tanzanians I love the way you guys got @diamondplatnumz back. But na hope mnavote kwenye bet website coz the kelele here doesn’t really count.
magazinequeendrika
Y’all. There is nothing you can say to convince BET to get this man to perform. They made this decision months ago, so stop trying!!!!!
Katika hatua nyingine, kituo cha redio cha Kenya cha Home Boyz Radio jana kilitaka kujua muziki wa nani kati ya Diamond na Davido unaopendwa zaidi na Wakenya. Tweets hizi zinaongea zenyewe.

TUMEAMIA HUKU