Featured Posts

Tuesday, June 17, 2014

JOKATE AIBUKA NA UBUNIFU MPYAAAA, DAH NI SHIDA CHEKI HAPA UJIONEE MWENYEWE

MWANAMITINDO Jokate Mwegelo ameibuka na ubunifu mpya wa sabuni ya kuogea inayokwenda kwa jina la Mo hiyo ikiwa ni baada ya kutesa na bidhaa ya ndala.
Mwanamitindo Jokate Mwegelo.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Jokate alisema uzinduzi wa sabuni hiyo unatarajiwa kufanyika leo Jumatano, Juni 18, mwaka huu ambapo yeye na timu yake watatembea kwa miguu kutokea mjini (Posta) kuelekea Mbagala huku wakigawa zawadi kwa akina mama.
“Nashukuru nimeweza kubuni tena bidhaa nyingine, nataka kuwaambia wasichana wenzangu, wasilale. Tukitaka tunaweza kufanya makubwa. Nawashauri wapenzi wangu wakae barabarani kunisubiria nitapita na kundi langu la Kidoti ili niwapatie zawadi,” alisema Jokate.
Jokate Mwegelo.
Jokate amekuwa akibuni mitindo mbalimbali kama nguo, nywele na ndala lakini pia ni mwigizaji wa sinema za Kibongo.

TUMEAMIA HUKU