Featured Posts

Friday, July 4, 2014

BAAMEDI AMGONGA MUUZA MAHINDI AKIFUNDISHWA GARI, SOMA ZAIDI HAPA

UZEMBE! Josephine Josin (19), mkazi wa Morogoro ambaye anafanya kazi ya uhudumu wa baa iliyopo maeneo ya Mji Mpya, mkaoni hapa, amedaiwa kumgonga na gari muuza mahidi aliyefahamika kwa jina la Pori wakati akifundishwa gari na mpenzi wake.
Gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 636 CVE lililopata ajali.
 Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo dereva wa gari aina ya Toyota Noah lenye namba T 63* CVE, Alfa Ibrahimu alikuwa akimfundisha Josephine ndipo alipomgonga Pori.

...Mahindi yakiwa yametapakaa eneo hilo baada ya ajali.
 “Awali tulimshuhudia huyu baamedi akinywa pombe na huyu dereva wa Noah, baada ya kufunga baa majira ya saa 3 usiku, akaingia kwenye Noah akaendesha huku akiwa amelewa na dereva aliyekuwa akimfundisha (Alfa) naye alikuwa amelewa.

Wazee wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakichukua maelezo kutoka kwa Bw. Alfa Ibrahimu na Josephine Josin ambaye ni baamedi kuhusu ajali hiyo.
“Tuliwatazama tu lakini ghafla alikanyaga mafuta kwa nguvu na gari ikaruka na kumvaa mzee anayeuza mahindi (Pori) na kutokea upande wa pili ikagonga bucha langu,” alisema Mazengo.
Bucha la Bw. Mazengo lililopata kashi kashi hiyo.
 Akizungumza na mwandishi wetu mara baada ya kutoka hospitali alipolazwa kwa muda, mzee Pori alisema alipata majeraha madogo katika paji la uso na wahusika walimfuata na kumlipa Sh 40,000 kama gharama za matibabu pamoja na mtaji wake wa mahindi.

Mzee Pori anayefanya biashara ya kuuza mahindi akiwa na majeraha katika paji la uso.
 Akihojiwa na mwandishi wetu kuhusiana na tukio hilo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao alikiri kutokea kwa tukio hilo ila akasema yeye si msemaji, aulizwe Kamanda wa Polisi wa Mkoa ambaye hakuweza kupatikana mara moja.

TUMEAMIA HUKU