Featured Posts

Wednesday, June 11, 2014

BREAKING NEWS, MAJAMBAZI YAVAMIA KITUO CHA POLISI NA KUMKATAKATA MAPANGA ASKARI PAMOJA NA MGAMBO

Tukio hilo limetokea usiku wa saa nane katika Kituo cha Polisi Kimanzichana ambapo askari walikuwa lindo. Wakaja watu kama wanne hivi kwanza wakiwa na mwenzao ana bandeji akijifanya majeruhi wamekuja kuchukua PF3 wakamtibie. Kumbe ni majambazi wana mapanga wameyaficha kwenye makoti. 

Ghafla wakaanza kuyatoa na kuwashambulia askari na mgambo waliokuwa kituoni. Askari Ngonyani ambae sasa ni marehemu alijitahidi kupambana nao lakini alizidiwa nguvu na kumkata kata kwa mapanga pamoja na mgambo wawili waliokuwa kituoni hapo. 
Baada ya tukio hilo, majambazii hayo yalipora bunduki mbili za poliso aina ya SMG na Magobore mawili yaliyokuwa yakihifadhiwa kituoni hapo. 

Nje kulikuwa na sakari mmoja wakike alikuwa nje kwenye gari alijificha kwa kuwa hakuwa na silaha muda huo, na ndiye aliyetoa taarifa kituo kikuu cha Mkuranga mjini kwa OCD.

Bw. Ngonyani alifia hospitali ya wilaya akipatiwa matibabu, na mgambo wawili wanaendelea na matibabu, ila mmoja hali yake imekuwa mbaya na amehamishiwa Muhimbili.

TUMEAMIA HUKU