Featured Posts

Thursday, April 17, 2014

JOHARI: HARUSI YA RAY NITAKUWA MWANDAAJI CHAKULA

Na Erick Evarist
MKONGWE kwenye sanaa Bongo, Blandina
Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa endapo
ikitokea mkurugenzi mwenzake, Vincent Kigos
akaoa, yeye atajitolea kuwa mwandaaji wa
chakula.
Akizungumza na mwanahabari wetu mwishoni
mwa wiki iliyopita, Johari alisema yeye na Ray ni
watu wa karibu kwa kuwa wameiongoza kampuni
yao kwa muda mrefu hivyo katika jambo muhimu
kama la ndoa, lazima ajitoe kinaga ubaga
kufanikisha.
“Yani hata kama ikitokea kesho mkasikia Ray
anaoa ujue kabisa nitakuwa muandazi kuhakikisha
madikodiko yanawafikia waalikwa kwa wakati
muafaka,” alisema Johari ambaye mara zote
amekuwa akikanusha kuwa uhusiano wa
kimapenzi na Ray.
GPL

TUMEAMIA HUKU