Featured Posts

Saturday, April 12, 2014

JAY DEE AOMBA RADHI KWA KUAHIRISHA SHOW YA UZINDUZI KWA AJILI YA MAFURIKO

Mvua inayoendelea kunyesha kwa wingi katika
eneo la Dar es Salaam na maeneo mengine nchini
imeripotiwa kusababisha athari kubwa ikiwa ni
pamoja na uharibifu wa makazi na miundo mbinu.
Hali hiyo imemlazimisha Lady Jay Dee kuahirisha
uzinduzi wa audio na video ya wimbo wake mpya
alioupa jina la Nasimama.
Lady Jay Dee ametangaza kupitia ukurasa wake
wa Facebook na kuambatanisha na picha ya jinsi
eneo hilo lilivyoathiriwa na mvua.
Nasikitika kutangaza kuahirishwa kwa shughuli ya
utambulisho wa wimbo na video mpya ya Jaydee
'NASIMAMA'. Kutokana na hali tete ya bojo
iliojitokeza ambayo iko nje ya uwezo wa
binadamu.. LAKINI Wimbo na Video vitarushwa
LEO ktk mtandao. Çds na DVD vitasambazwa kwa
walengwa((Media)) hapo kesho na Jumatatu.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote
uliojitokeza....JayDee

TUMEAMIA HUKU