Featured Posts

Saturday, April 12, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUVUNJWA KABURI LA SHEIKH YAHYA HUSSEIN NA SHEIKH KASIM

Ndugu Wanahabari,
Assalam Aleykum
Kama mnavyojua kwamba kumetokea tukio la
kusikitisha la kuvunjwa kwa Makaburi ya
Masheikh Wetu, wapendwa wetu , wazazi wetu
na viongozi wetu wa Dini ya Kiisalam ,
Marehemu Sheikh Yahya Hussein Na
Marehemu Sheikh Kassim Bin Juma, Usiku wa
kuamkia tarehe 10 /4/2012 katika viwanja vya
Makaburi ya Tambaza Jirani na Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Tukio hili , licha ya kusikitisha lakini
limeziingizia fedheha Familia hizi mbili za
Masheikh Hawa na Kwa Waisalamu kwa
Jumla . Kwa Desturi na Sheria , Viwanja vya
Makaburi ni mahala panapotakiwa
Kuheshimiwa kutokana na ukweli kwamba ni
moja wapo ya sehemu za Ibada .
Hivyo basi kutokana na Tukio hilo ni dhahiri
kwamba waliofanya kitendo hicho wamekiuka
mafundisho ya Dini ya Kiislamu na hivyo
kutenda kosa ambalo kiimani linaweza
kusababisha Madhara Makubwa kwao
wenyewe , Jamii na Taifa kwa Jumla .
Kwa muktadha huo basi Familia ya Marhum
Sheikh Yahya Hussein imeumizwa kwa
kiwango cha juu na tukio hilo hasa
ikizingatiwa kuwa Makaburi yaliyovunjwa ni la
baba yetu na la aliyekuwa swahiba wake
mkubwa Mzee wetu Sheikh Kassim Bin Juma
Pekee.
Hali hii inaonyesha kwamba kuna Chuki
Binafsi , Udhalilishaji na Njama za Kuhujumu
familia yetu , Dini yetu na Waislamu kwa Jumla
na hivyo kitendo cha aina hii kinaweza
kuliingiza Taifa katika migogoro isiyo na Tija ,
kidini , Kisiasa, kiuchumi na kimaendeleo ya
Jamii .
Hata hivyo Familia ya Marhum Sheikh Yahya
Hussein imefarijika kuona uongozi wa Serikali
ya Mkoa wa Dar es salaam Pamoja na Baraza
Kuu La Waisalamu wa Tanzania ( BAKWATA )
chini ya Mufti wa Tanzania Sheikh Mkuu Issa
Bin Shaaban Simba kulishughulikia kwa
haraka suala hili katika mawanda ya
kuthamini, Mila , Desturi na Ibada za Makaburi.
Hatua hiyo inaonyesha ni jinsi gani Jamii
nzima ilivyoguswa na kadhia hiyo ambayo
inahatarisha Usalama wa Nchi na raia kwa
sababu Waumini na wananchi wengine ambao
ni wapenzi wa Viongozi hao wa Kidini
wanaweza, kutokana imani zao , kujichukulia
sheria mikononi .
Hata hivyo uongozi wa Serikali Mkoa wa Dar
es salaam na vyombo vyake bado unatakiwa
kuwa makini katika maagizo yake na
utekelezaji wa kazi zake hasa katika sehemu
ambazo zinagusa hisia za watu kama
Makaburi na sehemu za Ibada ili kuepuka
matukio yenye sura ya Hujuma kama tukio hilo
la makaburi ya Tambaza ambayo yanaweza
kuleta mtafaruku ndani ya jamii na kuvunjika
Amani ya nchi .
Sisi kama Familia Ya marehemu Sheikh Yahya
Hussein tunaiomba Serikali na vyombo vyake
iwasake na kuwachukulia hatua kali za
kisheria wale wote waliohusika na hujuma
hizi .
Pamoja na hayo familia inaona kwamba dawa
ya kuepukana na matatizo kama haya ni
kujenga uzio katika eneo hilo ili kuhifadhi
Makaburi hayo . Kwa hiyo tunaiomba Manispaa
ya Wilaya ya Ilala ijenge uzio katika eneo la
Makaburi ya Tambaza .
Kwa upande wetu , pamoja na nia nzuri
ambayo Serikali imeonyesha ya kutaka
kuyajenga tena Makaburi hayo , lakini sisi
kama Familia ya Sheikh Yahya Hussein na
Sheikh Kassim Bin Juma tumeamua kwamba
tutajenga Makaburi ya wazazi wetu kwa
gharama zetu wenyewe .
Wabillahi Tawfiq
Alhajj Maalim Hassan Yahya Hussein
( Kwa niaba ya Familia )

TUMEAMIA HUKU