Featured Posts

Tuesday, April 15, 2014

ALICHOSEMA JUX BAADA YA UMBEA KUZAGAA KUWA AMEFANYA VIDEO NA JACK CLIFF

December 2013 zilitoka stori kwamba Mtanzania
Jackie Cliff ambae ni mrembo aliewahi kutokea
kwenye video kadhaa za wasanii wa bongofleva
amekamatwa na dawa za kulevya huko China.
Jackie Cliff ni mpenzi wa msanii wa bongofleva
aitwae Jux ambae amehojiwa na Gossip Cop
Soudy Brown baada ya picha kadhaa kusambaa
akitengeneza video yake mpya huko China na
mrembo ambae hajaonekana sura, ishu ambayo
imefanya wengi wahisi kwamba ni Jackie Cliff.
Jux amekanusha stori kwamba hivyo video
amefanya na Jackie Cliff na kusisitiza kwamba
kutomuweka Jack kwenye hiyo video ni kutokana
na sababu zake binafsi na wala hataki
kuzungumza zaidi kuhusu hizo ishu.
Namkariri akisema ‘siwezi kusema ila kama
atakuepo kwenye video au hatokuepo… ni watu
wenyewe wataona’
Kwenye sentensi nyingine Jux amekanusha stori
za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Vanessa
Mdee ‘V money’ kwamba ni rafiki yake tu ila
hakuna kingine cha zaidi’

TUMEAMIA HUKU