Featured Posts

Thursday, April 17, 2014

MAJIRANI WAMLALAMIKIA JIDE KWA UCHAFU

Gladness Mallya na Hamida Hassan
MAJIRANI wanaoishi karibu na mwanamuziki wa
kizazi kipya Bongo, Judith Wambura ‘Jide’
wamelalamika kwamba mwanamuziki huyo
ameiweka nyumba yake katika mazingira ya
uchafu yanayohatarisha maisha yao.
Wakizungumza na Amani, majirani hao wanaoishi
Kimara-Temboni jijini Dar, walisema mwanadada
huyo ameacha vichaka vikubwa vinavyoizunguka
nyumba yake hali ambayo ni hatari kwani nyoka
wanaweza kufanya makazi hivyo kusababisha
maafa kwa watoto na watu wazima.
“Yaani huyu mwanamuziki Jaydee ametuachia
kichaka, yeye na mumewe hawataki kufanya usafi
kuizunguka nyumba yao hali ambayo inatupa
wasiwasi sisi majirani, tuna watoto wanaweza
kung’atwa na nyoka kwani nyoka hupenda
kuzaliana kwenye vichaka kama hivi,”
alisema jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa
jina lake gazetini.
Waliendelea kusema kuwa, Jide hana hausigeli
wala ndugu yeyote anayeishi naye, inawezekana
ndiyo maana anashindwa kufanya usafi kuzunguka
nyumba yake.
“Lady Jaydee anaishi na mumewe (Gardner) tu
labda ndiyo sababu ya kushindwa kutunza
mazingira, majani yameota mpaka kero.
Tumeshapeleka malalamiko yetu serikali ya mtaa
lakini hajaitwa kuambiwa, tunashangaa,” alisema
jirani huyo.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili
lilimtafuta Jide na mumewe Gardner ambapo
mume huyo ndiye aliyepatikana na kusomewa
madai hayo. Baada ya kusikiliza mpaka mwisho,
Gardner alijibu:
“Kama wamesema hivyo mimi sina la kujibu (no
comment)”.
Juzi, mapaparazi walifika kwenye ofisi ya serikali
ya mtaa lakini ilikuwa imefungwa.
GPL

TUMEAMIA HUKU