Featured Posts

Thursday, April 17, 2014

MASKINI:SOMA MESEJI ZA WATU WALIOKUWA KWENYE MELI KWENDA KWA NDUGU ZAO WAKATI MELI INAZAMA

Meli ya Korea Kusini iliyokua imebeba zaidi ya
abiria 460 wengi wakiwa ni Wanafunzi, ilizama
kusini mwa pwani ya nchi hiyo siku ya Jumatano
asubuhi ambapo mpaka sasa wengi
hawajapatikana huko Korea Kusini ilikozama na ni
siku moja tu baada ya ajali ripoti zimeanza kutoka
za msg zilizotumwa na wale waliokuwa
wamekwama ndani ya meli hiyo.
Mwanafunzi:’huenda hii ndio mara yangu ya
mwisho kukuambia kuwa nakupenda,’ndio
ulikuwa ujumbe wa mwanafunzi mmoja kwa jina
Shin Young-Jin kwa mamake.
Mama:”na mimi nakupenda mwanangu,” alijibu
mama yake Shin kwa ujumbe wa simu bila kujua
kilichokuwa kinaendelea.
Kulingana na jarida la Herald nchini humo, Shin
alikuwa miongoni mwa watu 179 waliookolewa
lakini wazazi wengine waliopokea ujumbe kama
huo bado hawajaweza kuwaona watoto wao.
Mawasiliano mengine kati ya mwanafunzi mmoja
na babake , yalinukuliwa na shirika la habari la
AFP ni haya hapa chini
Mwanafunzi: “baba usijali,nimevaa boya la
kujiokoa na niko na wasichana wenzangu. Tuko
ndani ya meli na bado hatujaanza kuokolewa.”
Baba: Najua msaada uko njiani,lakini kwa nini
hamjaanza kuelea, tafadhali jaribu kuondoka ndani
ya meli kama unaweza.”
Mwanafunzi: ”Kuna msongamano mkubwa na
meli tayari imeanza kuzama”
Mwanafunzi aliyetuma ujumbe huu bado
hajapatikana.
Familia za abiria waliokuwa ndani ya meli hiyo
walijawa na hisia wakisubiri taarifa zozote kuhusu
wapendwa wao.
Katika ujumbe mwingine wa simu, mwanafuzni
mmoja alimtumia ujumbe kakake mkubwa meli
ilipoanza kuzama.
Mwanafunzi: “meli imekwama na haisongi walinzi
wa baharini wameanza kuwasili kujua hitilafu
imetokana na nini’
Kakake:” usiwe na wasiwasi fanya kila
mnachoamrishwa kufanya na kila kitu kitakuwa
shwari.’ baada ya hapo hakukua na mawasiliano
mengine yaliyoendelea.

TUMEAMIA HUKU