Featured Posts

Wednesday, May 7, 2014

HUYU NDIYE MWANAMKE ALIYENISHANGAZA SANA ....HARIDHIKI BANA HATA KIDOGO


Nina mpenzi wangu anayefanya kazi Morogoro, mwezi march alikuja kunitembelea sababu alikuwa likizo na alikaa kwangu wiki 2 na siku 3 tangu afike. Alishikwa na malaria kali ikabidi niombe ruhusa kazini ili nimuuguze.

Kiukweli nilimpa kila kitu anachotakiwa kupewa mgonjwa including dawa,vyakula vilivyopendekezwa na daktari na vyakula alivyopenda mgonjwa, pamoja na gari kumpeleka hospitali au sehemu yoyote aliyopenda ili kumliwaza mgonjwa. Mungu akasaidia akapona na amerudi morogoro.

Lakini cha ajabu juzi ananiambia sikumjali alipokuwa anaumwa sababu sikuwahi kumletea kadi ya get well soon pamoja na Mauwa kama wenzake wakiumwa wanavyofanyiwa. Ebu nisaidieni kadi na maua tu ndio mtu akujali?

TUMEAMIA HUKU