Featured Posts

Wednesday, May 28, 2014

MAMA ANA TIBAIJUKA SASA AKALIA KUTI KAVU BUNGENI

Bajeti ya Wizara ya Ardhi na Makaazi iko katika ati ati ya kupitishwa na bungeni leo hii. CCM baada ya kupima upepo wameita wabunge wao mapema wakutane baadae ili kuokoa jahazi.

Hotuba ya waziri prof..Tibaijuka ambayo imekuwa tofauti kabisa na ile ya kamati ya bunge juu ya wizara hiyo. Hotuba ya kamati imekuwa chungu mno.Imeibusha uozo mwingi ndani ya wizara.

Aidha, kama haitoshi hotuba ya waziri kivuli kwa wizara hiyo mh.H.Mdee imeanika ufisadi mkubwa ndani ya wizara hiyo,hususan kwenye suala la kigamboni na chasimba mkoani Dar es Salaam.

Pia,wabunge wengi wanaosimama wanasema hawaungi mkono hoja ya waziri. Kwa jumla,prof.Tibaijuka leo maji yamemfika shingoni.

Hata hivyo,kwa kuwa wabunge watetezi wa ufisadi na wanafiki wameitana basi wote tunatarajia wataufyata.Mikia yao wataiweka katikati ya miguu kama mbwa mwoga afanyavyo


TUMEAMIA HUKU