Featured Posts

Thursday, July 24, 2014

VIDEO QUEEN WA LINEX ATISHIWA KUUAWA, KISA KUZAA NA MPENZI WA MTU

Stori: Hamida Hassan
Video Queen wa mwanamuziki Sunday Mangu ‘Linex’ aliyeng’arisha Wimbo wa Ifola, Janeth Bundala amedai kutishiwa maisha na mfanyabiashara mmoja aliyemtaja kwa jina la Johari Ali, kisa kikiwa ni kuzaa na aliyekuwa mpenzi wake.
Akizungumza na Ijumaa katika ofisi za gazeti hili, Janeth alisema mama huyo ambaye anamheshimu sana hakutarajia kama angeweza kumtishia maisha wakati mwanaume anayetajwa alishaachana naye.
“Yule mwanaume niliyezaa naye ni kweli alikuwa mpenzi wa yule mama lakini walishaachana, sasa nashangaa ananitumia sms za vitisho.
Nimekwenda kutoa taarifa polisi na kumfungulia jalada la kesi lenye namba KJN\RB\6333/14, chochote kitakachonikuta ataisaidia polisi,” alisema Janeth.
Ijumaa lilimpigia simu Johari na kumsomea mashitaka yake ambapo  alisema yuko China na hamjui Janeth.

TUMEAMIA HUKU