Featured Posts

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Showing posts with label SIMULIZI. Show all posts
Showing posts with label SIMULIZI. Show all posts

Monday, June 9, 2014

SIMULIZI NA KISA CHA KWELI, "KUPENDA KULINIPONZA " IFATILIA UPATE UHONDO HAPA


Ndani ya gereza la segerea Robert anamsimulia rafiki yake Richie ambae ni mwandishi wa habari kuhusu kesi yake ya mauhaji.
Ilikuwa mwaka jana mwezi wa kumi na mbili siku ya sikukuu ya x-mas .Nilikuwa na kipenzi change Queen chumbani ,nikamuuliza swali.Ujue nakupenda sana Quen?Hata mimi nakupenda Richie .Nitaamini vipi kama kweli unanipenda ?Sitokuacha mpaka fedha zako zitakapoisha.Ahaa , Queen ina maana unanipendea pesa?Ehee babu ,kwani ulikuwa ujui ?Mwanaume pesa ,suruali hata wanawake tunavaa.Ahaa Queen unasemaje ?Ehee ni mambo y a digital hayo tushaama analogy siku nyingi pesa kwanza mapenzi yanafuata.


Nilisikia kama mshale umeuchoma moyo wangu ,maumivu niliyoyapata sijui nisemeje.Nikabaki nimeduwaa huku nikishika moyo wangu na kujiuliza moyoni.Queen yule niliyekutana nae kijijini Lamadi Mwanza nilipokwenda kwenye harusi ya mjomba ,babu yake aliponiona akaniomba nimsaidie mjukuu wake kwenda Dar e salaam akatafute maisha kwani maisha ya kijijini ni magumu ,nikakubali.Aliponionyesha mjukuu wake hakika alikuwa ni mzuri ila uzuri wake ulifichwa na kumezwa na umaskini pamoja na maisha magumu ya kijijini pale nilimpenda palepale.Nikaongea na wazee Queen awe mchumba wangu wakakubali na nikakamilisha taratibu zote na kumchumbia Queen na kuondoka na Queen mjini .Cha kwanza ulipofika mjini nikampeleka saloon akapigwe soapsoap hakika alivutia kila mtu alimsifia .Nikamuanzisha masomo ya sekondari katika shule binafsi kwa maana muda huo alikuwa na miaka 16 na mimi miaka 26 tukawa tunaishi kama mke na mume ingawa ni kosa kisheria.Baada ya kumaliza kidato cha sita nikampeleka Havard university Marekani akasomee shahada ya kwanza ya utawala wa biashara.Ili kumuonyesha ni jinsi gani nampenda alipohitimu Havard nikampeleka Australia akasomee shahada ya pili ya utawala wa biashara.Alipohitimu na kurudi bongo nikamnunulia kampuni ya clearing and forwarding ahisimamie yeye,ikamnunulia na gari ,nikajenga nyumba mpya ya kisasa Tegeta,nikanunua na mashamba 3 pale Kibaha kwani nilijiona sasa natarajia kuwa baba wa familia na kuandika jina lake katika hatimiliki vya vitu vyote kumuonyesha ni jinsi gani ninavyompenda kwani nilijua ni mama wa watoto wangu mtarajiwa kwani mda si mrefu tungefunga ndoa .Looh Queen ananijibu hivi leo ?Rafiki yangu Samwel aliniambia Queen ana mwanaume mwingine ambae ni mkurugenzi wa fedha benki kuu ya Tanzania(BoT) kwani huwa anawaonaga New African Hotel mara kwa mara yeye akiwa anafuatiliaga malipo yake ya kupelekaga tenda ya magunia ya mchele hotelini hapo.Nikafanya uchunguzi kwenye simu ya Queen nikakuta ameweka password nikamvizia siku moja usiku amelala nikaichukua simu yake na kuna fundi simu niliwasiliana nae pindi nitakapoipata simu ya Queen basi aje haraka nyumbani kwangu aiondoe password , nikampigia aje .Fundi alipofika akaondoa password na nikayaona mawasiliano ya Queen na mkurugenzi wake na siku inayofuata walikuwa na miadi ya kukutana kule hotelini saa 9 alasiri, aisee moyo uliniuma sana baada ya hapo fundi alinishauri ili Queen asijue kama tumeondoa password katika simu yake basi tuipasue kwa kuindondosha chini na isiweze kuwaka tena ,nikafanya hivyo na kuipeleka chini ya kitanda sakafuni ikionekana imedondoka kutoka kitandani.Kesho yake ambayo ni sikukuu ya x-mas nikamshtua Samwel ili tukashuudie.Laa haula kweli walifika pale wakiwa wamekumbatiana wakipigana mabusu motomoto ,kushikana shikana kwa sana ,denda nje nje .Mimi na Samwel tulikaa mwisho kabisa kwenye kona tukiona kila kitu kinachoendelea.Hasira na wivu zikapanda nikataka kuinuka nikawazuru Samwel akaniwahi na kiniambia tulia Robert mwanamke hapigwi dunia itampiga.Nilishindwa kuendelea kuvumilia kuwaangalia nikamwambia Samwel tuondoke tukapitia mlango mwingine wa nyuma na kurudi nyumbani nikiwa na hasira kuu na mawazo mengi .
Na mda hule ananijibu vile alikuwa amerudi kutoka kule hotelini akiwa amelewa nikazidi kushangaa Quen huyu huyu siku hizi ni mlevi wa pombe dah inauma sana.Nikamuuliza nikiishiwa pesa itakuaje ?Maihii jibu alilonipa “Nakuacha ,kwanza mimi ni mwanamke mzuri na mrembo bwana ,pili ni msomi na kila mwanaume ananitaka maskini kwa matajiri ila mimi ninaangalia pesa kwanza”.Aha ,nilijikuta nipo jikoni nikachukua kisu ,nikaenda stoo nikachukua panga na shoka .Niliporudi chumbani nikamkuta amelala kifudifudi ,nikainua shoka kwa nguzu zangu zote ikatua kwenye shingo yake, kichwa kule kiwiliwili kule damu chapachapa .Nikachukua panga nikamkata mikono ,mapaja ,miguu na kuviweka vipande vipande.Nikayashika makalio yake anayolingia nikachukua kisu nikakata minofominofu ,nikaja kwenye maziwa yake yaliyosimama kama embe nyonyo nikayakata yote .Nikatoboa tumbo lake lililo flat na kutoa moyo ,mapafu,maini,bandama na nikatia vyote kwenye kiroba .Kichwa nikmpeleke mjumbe wetu nyumbani kwake usiku huo huo miguu nikampelekea mama wawili jirani yangu,mapaja nikampelekea baba Koku muuza chipsi pale mtaani kwetu.Utumbo ,minofu ya makalio,mapafu,moyo,maini ,bandama nikampelekea bi Kidawa mwanamke mmbeya mmbeya sana pale mtaani.Kila niliyempelekea alishangaa na damu imetapakaa kwenye nguo zangu wakapiga makelele jamani kaua mtu huyo.Watu wakatoka majumbani ,wakanikamata na kunipeleka kwa mjumbe ,mjumbe akaamuru nipelekwe polisi.Kichapo nilichopewa polisi nikapoteza fahamu na kuja kuzinduka nikajikuta nikiwa mahabusu keko.Uchunguzi ulipofanyika nikaonekana nimeua kwa kukusudia na siku ya hukumu nikaukumiwa kifungo cha maisha jela.Robert analia kupenda kumemponza.
MWISHO.

SOMA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA YA MAPENZI

Kijana mmoja alitokea kumpenda sana dada mmoja ijapokuwa dada huyo alikuwa akimtolea nje mara kwa mara lakini kijana hakukata tamaa, akiendelea kurusha ndoano huku akiamini siku moja atafanikiwa.Siku moja dada huyo akiwa yupo nyumbani aliamua kumpigia simu huyu kaka na kumtaka aje nyumbani kwake, yule kijana alifurahi na kuhisi sasa ombi lake limekubaliwa. 
Akiwa nyumbani kwake dada huyo , alikuwa amevalia kanga moja laini, kutokana na hali ya hewa ya joto la Dar es salaam.Kwa upande wa yule kijana alikuwa amefurahi sana na haraka alijiandaa na kuanza safari kuelekea kwa huyu dada, njia ni kaka huyu alikuwa akijiuliza maswali mengi, huku akiwa haamini kama yule dada amemuita nyumbani kwake. Alipofika, alibisha hodi na yuel dada akafungua mlango huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake. 
Kaka huyu aliingia ndani huku kijasho kikimteremka mithili ya mtu aliyekuwa anakimbia. Dada huyu alimkaribisha vizuri, yule kaka aliomba maji ya kunywa huku muda wote akimtizama kwa umakini dada huyu mrembo, aliyeumbika kila idara na ile kanga nyepesi aliyovaa ilikuwa ikionyesha umbo zuri la dada huyu ambaye waswahili huwa wanasema, mtoto kajaaliwa (mashalaah) Kaka alikuwa akivuta pumzi kwa haraka haraka, na kusema "Nimefurahi sana, umenikaribisha nyumbani kwako ni pazuri sana." Yule dada alitabasamu na kusema "Asante sana, nimefurahi pia umeitikia wito wangu, samahani kwa usumbufu wangu".

Yule kaka alitabasamu huku akijisogeza sogeza "Hakuna tatizo, usijali kabisa, mimi nipo kwa ajili yako, naimani sasa nina...." Kabla hajamilizia kuongea yule dada alimshika mikono yake miwili huku akimtizama machoni, kwa macho yake malegevu, mithili ya mtu aliyekula kungu "Samahani kaka, mimi nimekuita hapa kuna jambo nataka unishauri, nataka kujua ni zawadi gani nzuri unaweza kumpatia mwanaume unayempenda" Kaka yule alikuwa akitetemeka na kusema "Chochote tu, zawadi ni zawadi, alimradi kuwe na mapenzi ya kweli" Dada yule alitabasamu na kusema "Ni kweli, mapenzi ya kweli ndiyo jambo la msingi kabisa , nitampenda maisha yangu yote katika shida na raha" Kaka yule akauliza "Utampenda? Nani huyo".

 Yule dada alitabasamu tena kwa tabasamu mwanana na kusema "Samahani, rafiki nilikuwa sijakuambia, wiki ijayo ndio nafunga ndoa na mpenzi wangu wa muda mrefu ambaye nampenda sana tena sana, na pia nilikuita ili nikupe kadi ya harusi, nitafurahi kukuona, kwani wewe ni rafiki yangu pia" Yule kaka alibaki amepigwa na butwaa, "Ati, nini unaolewa, daaah, jamani, kwahiyo." Alinyanyuka na kuondoka bila ya kuaga huku akimuacha yule dada anamuita ili ampatie kadi bila ya mafanikio.
SIYO KILA UNACHOKIWAZA MOYONI MWAKO KITATOKEA KAMA UNAVYOTAKA. KWAHIYO NI VYEMA KUJIANDAA KUKUBALIWA AU KUKATALIWA

Sunday, June 8, 2014

SOMA HADITHI HII YA KUSISIMUA YA "MIMI MWANANCHI" NI ZAIDI YA UTAMU ISOME HAPA

DALADALA imekolea mwendo. Kondakta wa daladala ametingwa kukusanya nauli. Pamoja na kutingwa kwake, bado hasahau kuwakumbusha abiria vituo.

“Manzese Darajaniiiii!”

“Shushaaa!” Abiria mmoja wa kike anapaza sauti.

Omi, dereva wa daladala hilo lililoanza kuchoka anakanyaga breki. Konda anafungua mlango, mama huyo anashuka. Kijana mmoja wa makamo anaingia ndani ya daladala hilo. Nyuma yake anapanda binti mwingine. Anakwenda moja kwa moja kuketi kwenye siti iliyo wazi, ambayo awali ilikaliwa na 


mama huyo aliyeshuka.
Hapa ni Igula Ilembula

Mtu huyo anapoketi tu, analegeza tai yake shingoni. Joto la Dar es Salaam si mchezo. Mchana huu jua linawaka kweli kweli, na kuwatoa jasho wakazi wake. Mabruki anailegeza vizuri tai yake na kuacha nafasi ya kutosha kuingiza hewani . 
Kisha anachukua nakala yake ya gazeti lililosheheni habari za kisiasa na kuanza kusoma kwa utulivu. Hana habari na yeyote ndani ya gari hilo. Akili yote ipo kwenye gazeti lake.

Pembeni yake anaketi kimwana mmoja. Tangu Mabruki aingie ndani ya gari hilo, binti huyo katingwa na simu yake ya kiganjani. Anaandika na kusoma ujumbe. Soga mtandaoni kwa mtindo mmoja. Mabruki wala hana hata habari.

Mara simu yake inaita. Anatulia kidogo kuusikilizia mlio wake. Mlio pekee unamtosha kumfahamu mpigaji ni nani. Huku mapigo ya moyo yakienda kasi, anaitoa simu hiyo iliyokuwa ndani ya mfuko wa shati lake na kuipokea. Anaongea kwa sauti ya chini ili kutowabughudhi abiria wengine.

“Helo my dear.”

“Baba Zahra za leo?”

“Salama tu mama. Kwema huko?”

“Kwema kabisa. Hofu juu yako mpenzi. Habari za Songea?”

“Njema mama. Bado tunaendelea na semina. Kesho tunategemea kumaliza kama nilivyokueleza. By Friday ntakuwa njiani honey.”

“Jamani baba Zahra usisahau basi kuninunulia viazi vya Songea. Shogaangu mama Hamdani kaniambia huu ndo msimu wake. Si unajua dear vilivyo bomba sana viazi vya Wangoni?”

“Yah!” Anaitikia. 
Mkewe anapata uwanja wa kumwaga sera. “Niambie basi honey, utaniletea? Halafu jamani huko ukibahatisha hata kakipande ka nyamapori dear. Si unajua sijala siku nyingi, tangu kipindi kile tulipoeta kwa mama Mngazi?”

“Tatizo upatilkanaji wake. Nitaulizia ulizia.”

“Halafu tena.”

Huyu naye! Mabruki anatamani kukata simu kabla konda hajaita kituo. Lakini mke wake anazidi kuzungumza pasi kuonesha dalili ya kukata simu haraka. Mambo ya Jirushe.

“Halafu tena honey, yule fundi uliyesema atufungie dishi wala hajaja kufunga. Mpigie basi umwambie afanye fasta. Si unajua tena nakosa kuangalia ze komedi?”

“Ok! Nitampigia. Basi ngoja nimpigie, kisha nitakupigia baadaye kidogo.” Mabruki anaona hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza maongezi kwenye simju.

“Utampigia hata baadaye kidogo. Halafu nilitaka kusahau kukwambia.”

Huyu naye, nini tena? Kwa hasira anajikuta anauliza, “nini tena?”

“Hivi yule shogaangu wa Mwanyamala yule alikuja nyumbani majuzi jioni si unamkumbuka?”

Mambo ya shoga zake na mimi wapi na wapi? “Ndiyo namkumbuka.”
Anajibu haraka haraka kumaliza maongezi.

“Basi mwenzangu kumbe shida yake yote iliyomleta nyumbani ilikuwa ni kukopa pesa. Hakutegemea kukukuta. Alipokukuta tu, akaishiwa sera. Basi leo kaja tena.”

Sijui nimkatie simu? Mabruki akashindwa kujijibu. Akabaki kimya.

“Basi mi namshangaa sana. Anapenda sana kuchonga juu ya maisha ya wenzake, kumbe naye anategemea vya kukopa.”

“Mh!” Mabruki akaishia kuguna. 

“Wala hata sijampa.”

Kabla hata hajajibu, anamsikia konda, “Shekilangooo?”

“Shushaaaa!”

Mabruki aliikata simu kama aliyewehuka ghafla. Mapigo ya moyo yakaruka mapigo. Jasho lilimtoka mithili ya mtu aliye jirani na tanuri la moto. 

Simu yake ikaanza kuita tena. Binti aliyeketi pembeni akishughulika na simu yake alikuwa akitabasamu kwa mbali. Dalili zote zilionesha alifanya jitihada za makusudi kuzuia kicheko chake kisitoke nje. Mabruki hakujisumbua naye. Akaonelea amwache ahangaike yake.

Akaitazama simu yake iliyokuwa ikiita kwa macho ya hofu tele. Mke wake hata hakuonesha dalili za kuchoka. Ilipokatika ikaita tena.

“Leggooo?”

“Shusha.” Mabruki akainuka haraka haraka na kushuka garini. Binti yule naye akashuka. Aliposhuka tu, akaenda haraka katika kibanda cha simu na kuzuga ananunua muda wa hewani.

Mabruki akaitazama simu iliyokuwa ikizidi kuita kwa mashaka tele. Kama atakuwa amesikia, itakuwaje? Ndilo swali lililomtawala. Akapiga moyo konde na kuipokea.

“Mbona ulikata jamani honey?” Mkewe alianza kwa lawama moja kwa moja.

“Mh eeh! Haina chaji ikazima.”

Upande mwingine jijini Dar es Salaam, mke wa Mabruki alitamani kuangua kicheko. Akaamua kuwa mstaarabu. Muda wote akizungumza kwenye simu, alikuwa ndani ya teksi. Alikuwa na haraka ya kufika mahali.

“Basi ukishaiweka chaji usisahau kunipigia mume wangu. Si unajua ninavyokumiss acha kabisa. Nakupenda sana.”

“Ok. Nami pia. Baadaye basi.”

Simu ikakatwa.

Mabruki akaenda moja kwa moja hadi ndani ya Leggo hoteli. 

Yule binti aliyezuga akinunua muda wa maongezi, akainyanyua simu yake na kuzungumza huku akicheka.

“Mbona umechelewa sweetie?” Kidawa alianza kumwambia Mabruki baada ya salamu.

“Foleni mpenzi.”

“Pole sana mpenzi wangu.”

“Ahsante. Si ushakula, twen’zetu ndani.”

“Ok. Tena nina hamu nawe. Maana umekwenda Manzese umechelewa.”

“Si wale mafundi wamenichelewesha. Ila fremu yako watu wanaisifia sana. Sipati picha utakapoanza kupanga vipodozi kwenye shelfu zake patapendezaje? Hadi nina wasiwasi vijana wa siku hizi watanipora.”

Mkono wake kiunoni kwa Kidawa. Binti yule aliyekuwa akizuga kununua muda wa maongezi, akawa kesha maliza kuzungumza kwenye simu. Akaingia pale hotelini na kuagiza soda ya Mountain Dew.

“Wala hani wangu. Akupore nani wewe mwenyewe upo juu kama roketi.”
Wote wakaangua kicheko.

Wakati wanachukua ufunguo wao mapokezi, binti yule aliwapita akiwa na chupa yake ya 
soda mkononi huku akizungumza na simu.

Wakaingia. Mabruki alikuwa ametoka hotelini hapo takribani masaa mawili nyuma. Hivyo akapitiliza maliwatoni. Akakoga. 

Kisha akaungana na Kidawa, mtoto wa mjini. Wakaanza kupeana mahaba.

“Ngo! Ngo! Ngo!” Mlango uligongwa wakati wao wakiwa wamezama katika bahari ya mahabadati.

“Nani?” Mabruki aliuliza kwa hasira na uchovu.

“Front office please. A minute please.”

Mabruki akamwashiria Kidawa akafungue.

Bibie Kidawa akavuta kipande cha kanga na kujisitiri japo kidogo. Akaenda mlangoni.
Akaufungua.

Wanawake wawili walikuwa wamesimama nyuma ya wanaume wawili, ambao nao walikuwa nyuma ya mhudumu wa hoteli.

Kidawa akapigwa na mshangao. Wale wanawake wawili wakapiga jicho moja kwa moja hadi ndani ili kuona kilichomo. Wakti Kidawa akiwa angali na butaa, akasukumiwa ndani mzima mzima. Kundi la watu wanne likaingia hadi ndani huku mhudumu akibaki koridoni pasipo kufahamu cha kufanya.

“Ndiyo Songea hapa?” Hilo ndilo swali pekee mama Zahra alilomudu kuliuliza. 

Mabruki akabaki akiwatumbulia tu macho wageni wale mithili ya mbwa aliyekabwa na mfupa.

Mama Zahara alipojaribu kuuinua mdomo wake kuzungumza, mdomo pekee ndio uliofunguka lakini sauti haikutoka.

Mara akaanguka chini akiwa amezidiwa na mapigo ya moyo. 

Kila mtu mle ndani akachanganyikiwa. Mabruki akavaa suruali yake kwa kasi ya ajabu. Jambo lililowashangaza wote, Mabruki ndiye aliyekuwa wa kwanza kwenda kumnyanyua mke wake. Akambeba mzimamzima mithili ya kuli na gunia la nafaka.

Alipofika chini, akaita teksi haraka na kumkimbiza hospitali.

MWISHO

HII NDIO BARUA KWA WATUMIAJI WANA FACEBOOK WOTE ISOME HAPA INANOGA BALAA


Kwako Kaka.

Usinione kwamba nimekaa kimya sana huku uswahilini ukaanza kusema kwamba nimekutenga, hapana, bado ninakukumbuka sana kaka yangu mpendwa. Toka ulipohama na kuhamia Masaki, nimekuwa mtu mnyonge sana, nashinda peke yangu huku simu uliyoniachia ikiwa mkononi mwangu.
Leo kaka ningependa kukuambia kitu kimoja, hasa mtandao huu wa Facebook ambao ulikuwa ukiniambia sana nisijiunge nao kwani nisingeweza kusoma. Niliyapuuzia sana maneno yako ila kwa sasa ndio naona madhara ya mtandao huu.
Leo nitakwenda kukuambia machache juu ya mtandao huu wa facebook ambao unatumiwa na simu zote zenye uwezo wa kuunganisha internet kama hii yangu, siwezi kuongelea kuhusu BBM kwa sababu sina Blackberry na wala siwezi kuongelea Whatsup kwa sababu sina simu yenye uwezo mkubwa, kwa sababu natumia Tecno kuingia facebook, acha niuzungumzie mtandao huu wa facebook.
Unakumbuka kwamba nilipokuwa kidato cha pili nilikuwa kichwa darasa zima, nakumbuka nilikuwa napata hesabu 90%, historia 98% na masomo mengine kwa alama za juu sana ila kwa sasa nimeshuka kwa kiwango kikubwa sana, sijui itakuwaje nitakapofanya mtihani wa taifa mwaka kesho.
Kaka jinsi nilivyofikiri kumbe si ukweli ulivyo. Kipindi cha mwanzo nilifikiria kwamba Facebook ni sehemu ya watu kuwa marafiki tu kumbe kuna mambo mengi sana ambayo hutokea nyuma ya pazia. Juzi juzi nilikuwa nimepata habari kwamba kuna msichana wa Kinaigeria kauawa, kisa facebook huku hata wengine wakiamua kutembea nje ya ndoa zao.
Unamkumbuka yule msichana wangu? Sasa hivi nimemuacha bhana eti kisa nimekutana na msichana mzuri huku Facebook, dah! Yaani sijui niseme nini kaka. Facebook imekuwa sehemu ya matatizo makubwa sana katika maisha yangu, muda wote naiwaza hiyo tu.
Kasi yangu ya kwenda kanisani imepungua kabisa na hata kama nitakwenda basi itakuwa ni lazima niwe nachati Facebook kisiri siri huku nikiweka post ya baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kanisani, kaka, niombee, hali si shwari kabisa.
Mpaka sasa hivi kaka ukiniuliza facebook imenipa faida gani, sina cha kujibu ila ukiniuliza hasara, zipo nyingi sana. Imenifanya hata kutokwenda kumsalimia dada, salio ambalo mara nyingi huwa unanitumia la shilingi 500 ili niwe nawasiliana na mama na kumjulia hali, mimi najiunga na huduma ya internet na kisha kuingia facebook.
Siku hizi usiku nimekuwa popo, nachelewa sana kulala na ninawahi sana kuamka. Tetesi za watu kufa, zote huwa ninazitolea humu, skendo za mastaa wengi huwa ninazitolea humu. Unakumbuka kipindi kile ambacho nilikwambia kwamba kama ningejiunga na Facebook marafiki zangu wangekuwa wazungu tu ili nipate bahati kama aliyoipata Baraka Kyomo ya kupendwa na mzungu wa Marekani na sasa hivi anakula bata? Mpaka leo mwaka wa tatu, sijampata mzungu yeyote.
Kuna matukio mengi sana huwa yanatokea humu kaka. Kuna mwanamke mmoja anaitwa Susan, huyu alikutana na mwanaume facebook, akazoeana nae sana na mwisho wa siku wakawa wapenzi. Mapenzi yaliendelea lakini Susan hakuwahi kuiona sura ya mpenzi wake anayechati nae, akalilia sana kuiona picha ya mpenzi wake.
Mwanaume huyo akamwambia sawa, ila usishtuke mara utakapoiona picha yangu nitakayoiweka, Susan akajibu sawa. Kaka huwezi kuamini, ndio maana nakwambia kwamba mtandao huu siku hizi hata mashetani nao wanautumia sana, baada ya mwanaume huyo kuiweka picha yake kwenye mtandao huu, Susan alipoiona tu, akaingiwa na mapepo ambayo baadae yakapelekea kuwa chizi na kugongwa na gari pale Magomeni Hospitali na kufariki papo hapo.
Ukiachana na huyo Susan kaka, kuna mwanaume mwingine anaitwa Pawasa ambaye alimpata rafiki wa kiume kutoka nchini Australia, wakawa marafiki sana, mwisho wa siku mwanaume yule akamtaka Pawasa aelekee Australia. Pawasa alifurahi sana, na kweli alipokwenda huko, akakutana na rafiki yake huyo ambaye alimtumia tiketi na kumpa barua ya mwaliko.
Kaka….kaka…kaka amini usiamini, baada ya kufika katika nyumba ya mwanaume huyo, Pawasa akapewa kinywaji kilichotiwa dawa, alipokunywa tu, akalewa na baada ya hapo kuingiliwa kimaumbile na huyo jamaa. Mungu wangu! Kwa sasa ninavyoongea, Pawasa kawa shoga mkubwa sana ambaye anajulikana sana nchini Australia.
Facebook imeniogopesha kaka, hasa hasa kwa hawa watu ambao hawataki kuweka picha zao na kila siku wanataka nichati nao. Huwa ninajiuliza sababu ambazo zinawafanya kutokuweka picha zao ni zipi lakini sipati jibu kabisa.
Maisha ya huku facebook yapo tofauti sana, kuna watu wanapenda sana sifa, utawakuta wengine wanasema wapo Samaki Samaki wanapata lunch na wakati wakati huo huo nipo nao huku Tandale. Na wengine wanadiriki kuandika wanasoma UDSM na wakati ni wafanyakazi wa ndani hapo Magomeni.
Ukiachana na hao wapenda sifa kaka, kuna wengine yaani wao wanajidai kuwa watawala, yaani utafikiri mtandao wa facebook ni mali yao kaka. Wewe unaweka picha halafu mtu anakuja na kukuambia itoe hiyo picha eti kisa hajaipenda, utafikiri nimemuwekea yeye, yaani maisha yao yamekuwa yakiwaambia kwamba wanatakiwa kuwa watawala kila kona.
Kaka…..kaka..kaka hivi unajua kwamba siku hizi hata biashara fulani fulani zimehamia facebook? Rafiki yangu Jumanne siku hizi wala ahangaiki kama zamani, akitaka tu, anamuinbox, wale wa kule kwa Macheni, Kinondoni wanakuja, yaani ni hatari sana kaka.
Kusema ukweli pamoja na mambo hayo yote lakini kwa asilimia chache facebook imeweza kunielimisha sana, imenifundisha kwamba ni watu wa aina gani ambao natakiwa kuwa nao. Wengine hawafai kaka, yaani wao kila siku wanaweka post kuhusiana na mapenzi, asubuhi mapenzi, mchana mapenzi na usiku mapenzi, kama watu hawa wakiwa marafiki zangu unafikiri na mimi nitakuwa mtu wa aina gani kaka, hauoni kama nitaweza kuwapenda mpaka binamu zangu na kuanzisha kizaazaa kwa mjomba?
Kaka, kama una lengo la kufungua akaunti facebook, achana nayo kabisa, ukija huku unaweza ukamuacha mke wako ndani ya mwezi mmoja tu, ukija huku unaweza ukawa unachelewa kulala kaka, ukija huku pia unaweza ukawa unapata makwazo kila siku, watu wengine wanakera sana.
Nitakuandikia mengi ambayo yanajili huku, ila hayo ni machache sana, siku nyingine, nitakuandikia tena. Utakapomaliza kuisoma hii barua naomba uichane kwani shemeji akiiona anaweza akamwambia mama kwamba nina akaunti facebook, si unajua mama akijua inakuwaje, ataweza kunipokonya hata hii simu ya mchina ambayo umenipa.
Naomba uwasalimie wote huko Masaki. Nimeamua kukuandikia barua na si kukupigia simu kwa sababu simu yangu haikuwa na salio la kutosha, 500 ambayo ulinitumia jana nilijiunga na internet ili niingie facebook. Nimeamua kukuandikia hii barua kwa sababu jana baba alisema kwamba leo angekuja kukutembelea, na ndio maana nimeandika na kumpa.

Siku njema kaka. Nitakuja huko pamoja na huyu msichana wangu wa facebook ili tuje tukusalimia kaka. Nakutakiwa siku njema. Mpe Hi Shemeji pamoja na mtoto wako, Junior.

SOMA SIMULIZI HII FUPI YA \ MTENDA HUTENDWA NI TAMU BALAA


Umaarufu wake pale chuo cha ualimu Butimba Mwanza, maumbile yake na sauti yake ilikuwa mitego tosha kwa wanaume kujisogeza karibu yake walau wapate kumsabahi kwa sababu yeye hakuwa na utaratibu wa kumsalimia mtu yeyote mpaka umuanze, na ilikuwa nadra sana kukujibu kwa maneno mara nyingi alitumia kichwa au kope zake kujibu salamu hizo, ndio waweza kusema kwamba ungekuwa wewe usingemsalimia lakini kiukweli alikuwa mzuri sana wa kuweza kukuvutia hata wewe, watu walimchukia lakini moyoni walimsifia kwamba alikuwa mrembo wa chati za juu sana.
Umaarufu wa kipekee wa binti huyu ulimfanya awe kama nembo ya chuo kwa wanafunzi, yaani ili uaminike kweli unasomea pale Butimba basi swali la kwanza la uthibitisho lilikuwa, “Unamfahamu Angel??”. Ukiwa unamfahamu basi kweli unaaminika unasoma chuo kile.
Hakuwa na pesa lakini alivyokuwa anaishi maisha ya juu mh! hutakaa huamini kwamba huko kwao analalia kitanda cha kamba na jamvi ndio godoro lake, huku ikimlazimu kusubiri giza liingie ndio aweze kuoga nyuma ya nyumba yao iliyoezekwa kwa nyasi kasoro chumba cha baba yake ambacho kiliezekwa kwa bati dogo lililochakaa.
Alizaliwa miaka ishirini na moja iliyopita kwa njia za kijadi na kupewa jina la Nyangoko alilokuwa nalo hadi anajitambua na baadaye kujijua na kugundua kuwa lile jina halikuendana na maumbile yake ya kupendeza lakini hakuwa na uwezo wa kulibadilisha lakini licha ya kushindwa kuibadilisha hali hiyo alitumia lazima pale chuoni na ole wako uthubutu kumwita jina hilo (Nyangoko) kama unataka usonywe hadi ujihisi upo uchi basi mwite Nyangoko badala ya Angel (enjo) au malaika kama alivyojibatiza mwenyewe na kulazimisha watu wamjue hivyo kwa hapo chuoni.
Angle alikuwa wakipekee!!!!
Watu walikuwa wanajiuliza kama alilazimishwa kusomea ualimu ama kufeli ndo kulimsukumia njia hiyo, hakika hakuwa akifanania!!!!!
Mguu wa bia uliobebwa na paja lenye unene wa haja, hipsi ambazo zilikuwa zikijibana vyema kwenye nguo zake na kuleta mvuto kumtazama, alijua kutembea vyema hivyo nyama za makalio yake zilitingishika vyema pia. Mwenye macho aliona!!
****
Deogratius au Mtu pori kwa wengi walivyomzoea sio tu kwa jinsi alivyokuwa mshamba hapana pia alikuwa anatoka Morogoro lilipotoka kundi lililovunjika la muziki wa kizazi kipya la watu pori lililopata umaarufu mwishoni mwa mwaka 2006.
Licha ya ushamba wake labda uliochangiwa na umaskini au mazingira aliyokulia Deo bado alikuwa na hisia kali za kimapenzi kama binadamu wengine na kikubwa zaidi alikuwa ameangukia katika kumpenda binti mwenye maringo na mikogo yote pale chuoni (Angel) na aliamua kuchuana vikali na Steward mtoto wa diwani kata ya nyamagana katika kumuwania Angel. Mchuano huo ulikuwa kama kituko kwani dharau aliyoonyesha Angle kwa Deo kwa mwanaume mwingine angekata tamaa au angempiga vibao yule binti.
“Hivi Deo ndugu yangu una marafiki????” siku moja katika maongezi yake na Deo aliulizwa
‘”Ndio ninao tena wengi tu mbona…..kwanini umeuliza hivyo ???’’ alijibu kwa furaha
“Basi rafiki zako wanafiki ``
``Kwa nini unawaita wanafiki nani huyo mnafiki ???``
"Deo hivi rafiki zako hawajakwambia huna hadhi ya kuwa na mimi? kaulize vizuri wakueleze" lilikuwa ni jibu alilopewa Deo siku alivyomwandikia kaujumbe Angle wakiwa darasani, darasa zima lilimcheka Deo.
Mtu mmoja tu ndio hakucheka nae ni Steward, hakupendezwa hata kidogo na dharau za Angel kwani aliamini Deo alimpenda Angel kweli tofauti na yeye aliyetaka kuonja ladha ya mrembo huyu kitandani kisha aachane naye . alijisikia vibaya pia kwa kuwa Deo alikuwa mwanaume na kijana mwenzake pia hivyo kuaibishwa kwa Deo ilimaanisha aibu kwa wanaume wote.
* * * *
Furaha aliyokuwa nayo siku hiyo hakuna aliyejiuliza kuna nini, Angel kwa mdomo wake alikuwa amemkubalia Deo kimapenzi , alikuwa amekiri makosa yake na kuomba msamaha na alimwomba waonane jioni hiyo guest moja pale jirani na chuo gharama juu yake Angel, kwa Deo hiyo ilikuwa furaha kubwa sana na hakuhitaji hata Angel aombe msamaha kwani alimwona yupo sawa tu na hana hadhi ya kumuomba msamaha.
Saa moja jioni tayari Angel na Deo walikuwa ndani ya chumba kimoja katika nyumba ya kulala wageni (guest), wote walikuwa na furaha huku Deo akiwa na hamu kubwa sana ya kuonja penzi la mwanamama huyu kwa malengo mawili tofauti, kwanza kuitafuta heshima alitambua wazi kwa kufanikiwa tu kulionja penzi la mwanadada huyu ataheshimika kwa tendo hilo la kumpiku mtoto wa diwani kwa kimwana huyu, pili aliamini kuwa Angel alikuwa anamfaa sana kuishi naye kama mke siku moja.
"Kaoge basi mpenzi wangu tupumzike kidogo nina hamu na wewe kweli," akiwa amebana pua Angel alimwambia Deo aliyekuwa pembeni yake, neno mpenzi ni kama lilipiga shoti akili ya kijana huyu kutoka shamba, kama mwizi haraka haraka akazama maliwatoni akimwacha Angel akisugua paja lake lililokuwa wazi kwasababu ya kinguo kifupi alichovaa. Paja lile sio tu lilikuwa laini bali pia ni kama liliongea lugha ya mahaba ambayo mwanaume akiisikia lazima atetereke.
"Atajua mimi ni nani na kamwe hatajutia usiku huu, tena ngoja cha kwanza nimalizie humuhumu nikaanze nae cha pili" alijisemea Deo huku akiendelea kujiosha mwili wake na kisha kujichua, alijihakikisha kabisa kuwa alikuwa ametakata mwili wake tayari kwa kugusana na mrembo Angel. Deo alikuwa kama mjinga ndani ya bafu, mara ajaribu staili atakazotumia akifika pale kitandani.
Baada ya kumaliza kuoga na kujifuta mwili wake vyema tukio ambalo lilichukua kama dakika kumi na tano, sasa Deo alitoka bafuni tayari kwa mapambano aliyokuwa amepania sana.
"Angel, Angel!"Deo aliita lakini chumbani hapakuwa na mtu wakati anatoka bafuni, Angel hakuwa pale ndani Deo aliangaza kama kuna chumba cha ziada pale ndani lakini hapakuwa na chumba kingine, akili yake ilisimama kwa muda hadi alipokutanisha macho yake na kikaratasi cha kalenda pale kitandani ambacho hakika kilimvutia kukisoma, kwa haraka haraka akakichukua.
“Au ametekwa mtoto wa watu…….dah!!!” alijiuliza Deo kabla ya kusoma yaliyoandikwa pale katika ile karatasi. Cha ajabu na kweli hapakuwa na maandishi yoyote yale zaidi ya tarehe mojawapo kuwa imezungushiwa duara nayo ilikuwa tarehe moja (1) ya mwezi wa NNE. Siku hiyo ya tukio.
Deo alijiuliza nini maana ya ujumbe ule. Mara ghafla akili yake ikapiga kama radi na kuleta majibu. Majibu yaliyomfedhehesha
"Ayaaaa leo siku ya wajinga mh!........ mi mjinga namba moja duniani,..yes!! mimi ni mjinga namba MOJA" aligutuka Deo baada ya kujiuliza na kupata maana halisi ya hiyo tarehe, mfadhaiko ulimkumba na kujikuta akivaa nguo zake kwa aibu kubwa japo alikuwa peke yake pale ndani. Alitazama kushoto na kulia hapakuwa na mtu. Hisia zake zilizokuwa juu sana zikafifiua na kupotea kabisa.
"Nitawaambia nini sasa washkaji ????? " alijiuliza Deo huku akivaa nguo zake.
Hakika alikuwa ameumbuka!!!!
* * *
Kwa furaha tele Angel alichukua tax iliyompeleka hadi ukumbi wa bwalo la magereza ambapo aliahidiwa na Steward kwamba amemwandalia zawadi kubwa sana siku hiyo. Tabasamu halikumuisha usoni kutokana na kituko alichomtendea Deo.
"Yaani ile ndio dawa yake hapo hatanisumbua tena nina uhakika….pumbavu kweli unadanganyika kijingajinga tu…..wapi na wapi mimi kulala na yule mlugaluga, yaani kweli kabisa aende kuninukia kimbuzimbuzi mimi!!!” alikuwa akijiwazia hivyo Angel wakati teksi ikiwa inazidi kuiacha barabara nyuma na kuelekea anapotaka Angel. Wakiwa wamekaribia kufika Angel alimwomba dereva apunguze mwendo ambapo alianza kujipamba uso wake hadi akapendeza kama ilivyo ada akajipulizia na marashi.
Kwa mikogo na manjonjo aliwasili ukumbini na mshehereshaji (MC) aliwanyanyua wageni wapatao 50 kumpokea mgeni rasmi ambao bila kinyongo walisimama na kuanza kumpigia makofi huku vigelegele pia vikisikika kuwatambulisha kina dada waliokuwa pale, kwa kitendo kile Angel alizidisha mikogo huku akitembea kama vile mlimbwende wa kimataifa alijisikia sana mrembo huyu.
Baada ya kufika na kuchukua nafasi yake kama alivyokuwa ameelekezwa na binti aliyewekwa kwa shughuli hiyo Steward alichukua kipaza sauti na kuanza kuzungumza.
"Ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana nachukua fursa hii bila kupoteza muda kumruhusu mpenzi wangu Angel mbele yenu afungue pazia hili na atoe zawadi yake niliyomwandalia kama ishara ya upendo wangu kwake, najua zawadi hii yaweza kuwa ndogo sana kulinganisha na pendo la dhati analonionyesha kwangu lakini naamini ataifurahia,baada ya kuifungua ndipo sherehe itaanza rasmi, napenda kutamka mbele yenu hakuna msichana nampenda kama Angel" aliongea Stewart kisha MC akamwongoza Angel kwa mbwembwe pamoja na fujo za Dj hadi kwenye pazia kubwa ili afungue na kutoa zawadi yake
"Kama sio gari mh!..........au kibajaji maana Sterwad naye….au ndo lile kabati kutoka Denmark alilokuaga ananiambia" alijiwazia Angel huku akizidi kutembea kwa mikogo kuelekea kwenye pazia. Aliamini alikuwa ni msichana mwenye bahati kupita wote duniani. Alitembea kwa pozi zote za kuzaliwa na za kuiga kwani aliamini ni wengi walikuwa wanamwonea wivu, hivyo alifanya kuwakomesha.
“Nawatakoma mwaka huu????!!!!!” alizidi kujishaua.
“Ntahesabu hadi tatu halafu atatufungulia pazia letu mwanadada mrembo Angel….sote tusimame ” Mc alisherehesha, kweli baada ya kuwa amehesabu hadi tatu, Angel akiwa na furaha tele alitelemsha lile pazia "1/4 HAPPY FOOLS DAY" ndio maneno makubwa aliyoyakuta mbele ya ukuta uliokuwa umezibwa na lile pazia
"Aibuuuuuuuu" ukumbi mzima ukazomea wanawake wakaanza kumshushua kwa kutumia mane, bila kuteleza akajikuta ameanguka chini alitamani azimie lakini hakuzimia, aliombea ardhi ifunguke aingie ndani yake lakini ndio kwanza ardhi ilikakamaa watu wote bila huruma wakaondoka wakamwacha hapo.
Alihaha huku na kule kama mfa maji!!! Aibu ikawa imechukua hatamu. Alikuwa amesahau kabisa aliyomtendea Deo muda uliopita sasa ilikuwa zamu yake!!! Naye ametendwa!!!!
Tena mbele ya umati mkubwa zaidi!!
Amakweli USILOPENDA KUTENDEWA NAWE USIMTENDEE MWENZAKO.

TUMEAMIA HUKU