Misukule ya Gwajima Yatinga Polisi.....Ndugu, Wazazi kuitwa ili kuthibitisha vifo vyao.
Baada
ya hivi karibuni kutoa waraka mzito unaowalenga watumishi wa
mungu kwa kile alichodai kuwa ni ukiukwaji wa sheria za mungu,
Nabii Hosea Chamungu ametangaza rasmi kuiwasilisha ripoti ya
misukule feki mikononi mwa jeshi la polisi ili hatua za
kisheria zichukuliwe....Akiongea kwa kujiamini, Nabii ChaMungu alimuonyesha mwandishi baadhi ya picha za misukule ikiwemo iliyowahi kuonyeshwa ndani ya kanisa la ufufuo na uzima linaloongozwa na mchungaji Josephat Gwajima..... "Unapofanya kazi ya mungu hutakiwi kuwa mwoga kwa lolote kwani yeye ndiye anayetulinda sisi sote, kondoo wa bwana wamekuwa wakipotea siku hadi siku huku wachungaji tukiwaangalia bila kuwaokoa.Mimi sikubaliani na hii miujiza ya kutoa misukule inayotangazwa kila siku wakati hatujui hao misukule walifia wapi....
"Baada ya kufunuliwa na mungu juu ya jambo hili, nimeanza kukusanya taarifa kuhusiaa na hili jambo na tayari uelekeo umeshapatikana, watu hawataamini siku nitakapoliweka wazi hili suala kwani nitaliomba jeshi la polisi liwashitaki wote waliorubuniwa na kujifanya misukule pamoja na wale walioinjinia ishu nzima.Kama kuna watu wenye uwezo wa kufufua watu kwa nini vifo vinaendelea kutokea kila siku?",alisema Cha Mungu.
Cha Mungu alidai kuwa zoezi hilo litafikia hitimisho mwishoni mwa mwezi ujao.
Aidha, alitoa wito kwa ndugu, jamaa na wazazi ambao kwa namna moja au nyingine wamehusika na kuficha siri za ndugu, jamaa au watoto wao waliojihusisha na zoezi la kumdhihaki Mungu la kujifanya wao ni misukule wangali wakijua si kweli wajisalimishe kabla hajawaumbua....
"Nitakapokamilisha details nitawataja kwa majina, mahali walipo na jinsi walivyohusika, kwa wale ambao wanaogopa vitisho waje nitawaombea na roho ya woga itaondoka na hakuna atakayewadhuru," alisema.
Jitihada za kumpata mchungaji Gwajima kuongelea suala hilo ziligonga mwamba kutokana na simu yake kutopatikana.