Kutoa pumzi mbaya ni tatizo linalowakabili watu wengi pasipo kujua chanzo ni nini.
Kila siku wanasafisha meno lakini bado harufu imegoma kuisha mdomoni wanapoongea au kupumua.
Leo tujaribu kujuzana japo kwa ufupi hali hiyo husababishwa na nini.
Tatizo hili kitaalamu huitwa Halitosis, huletwa na bakteria wanaotoa harufu mbaya kinywani.
Tunapokula
chakula,mabaki mengi ya chakula hujificha katika uwazi kati ya jino na
jino na mabaki mengine madogo sana hukusanywa katika ulimi.
Bakteria
hawa wanapokaa kwa muda maeneo hayo ,huzalisha kampaundi ya salfa
ambayo ndiyo chanzo kikuu cha harufu inayotoka mdomoni.
Na
pia aina ya chakula kama kitunguu chenye mafuta ya garlic ambayo
hufyonzwa katika mishipa ya damu na kupelekwa kwenye mapafu huzalisha
harufu mbaya wakati wa kupumua na pia hata uvutaji wa sigara huchangia
hili tatizo.
Hebu tuangalie njia chache tunazoweza kuzitumia ili kupunguza tatizo japo kidogo.
*Kusafisha kinywa(meno na ulimi) kila siku unapoamka kwa brashi nzuri na dawa ya meno ambayo ni salama.
*Unapomaliza kula piga mswaki, sukutua mdomo kwa maji mengi au chukua kipande cha uzi na pitisha katikati ya nafasi ya jino na jino ili kuondoa mabaki ya chakula.
*Kila
mara hakikisha mdomo wako haukauki mate, kwani mdomo mkavu hutoa harufu
mbaya. Hii ni kwasababu mate yana kemikali ambazo huua bakteria na pia
husidia kumeng'enya mabaki ya chakula mdomoni.
*Tumia bazoka zisizo na sukari nyingi kuzalisha mate pale unapoona mdomo wako ni mkavu.
*Pia unaweza ukamuona Daktari wa magonjwa ya kinywa ili asaidie kugundua chanzo cha tatizo ili kutibu.
Basi sisi wenye hili tatizo tujitahidi kulimaliza.
Mwisho
wa siku watu wako wa karibu, wanaweza wasikwambie kama kinywa chako
kinatoa harufu lakini ukajikuta unatengwa pindi unapotaka kuwasiliana
nao kwa karibu.
Maeneo
kama shuleni na vyuoni ambako wanafunzi wengi huunda vikundi vya
kujadiliana masomo utaona wewe unatengwa bila sababu za msingi na huleta
hali ya kunyanyapaliwa.