HILI kweli ni sekeseke la
Idd el Fitr. Wakati changudoa mmoja akinaswa na kumwagiwa maji na
wananchi waliochoshwa na vitendo vya ukahaba vinavyofanywa jirani na
makazi yao, msichana mwingine aliokotwa akiwa amelewa chakari na
kudhaniwa kuwa na mapepo, maeneo ya Sinza Afrikasana jijini Dar Jumanne
hii.
“Yaani tumechoshwa na hawa machangudoa, inafikia hatua tunashindwa kulala kwa sababu ya miguno yao ya kimapenzi, hata watoto wanashtuka usingizini kwa sababu ya mambo hayo, ni hatari kwani wanaweza kujifunza ufuska, tumeamua kuwanasa leo jamani na itakuwa fundisho kwao,” alilalamika mmoja wa majirani hao.
Huku timu ya Operesheni Fichuo Maovu (OFM) ya Global Publishers ikiwa ‘beneti’ na majirani hao, ilishuhudia wawili hao wakikamatwa na kupewa adhabu ya kulowanishwa kwa maji ya moto ambapo nguo zao zililoa chapachapa.
Wakati changudoa huyo akipewa adhabu hiyo
ili liwe fundisho kwa wenzake wanaokesha pembezoni mwa barabara ya
Shekilango, msichana mwingine anayedhaniwa kuwa alilewa kupita kiasi,
alikutwa akiwa amezungukwa na watu nje ya baa maarufu ya Corner.Changudoa huyo akijuta baada ya tukio hilo.
Kundi kubwa la watu lilimzunguka mwanamke huyo kutokana na vitendo
vyake kuashiria alikuwa amelewa bwii, wengine wakiamini alikuwa na
mapepo hivyo kutaka kujua namna ya kumsaidia.“Huyu dada jamani itakuwa majini yake tu yanamsumbua, si unajua watu wengine majini yao hayapendezwi na ulevi uliozidi kiwango, maana mtu mwenyewe haeleweki, tukimshika kumsaidia anataka kuturukia sasa sijui tufanyaje,” alisikika kijana mmoja akisema.
Hata hivyo, baadhi ya vijana waliokuwa
eneo hilo walionekana kupanga mbinu za kumchukuwa msichana huyo na
kwenda kumfanyizia, kitu kilichoshtukiwa na mabaunsa wa baa hiyo ambao
walimpandisha kwenye Bajaj na kumkimbiza Kituo cha Polisi Mabatini
ambako baada ya askari kuwasikiliza, walishauri apelekwe hospitalini.Binti anusurika kubakwa baada ya kulewa chakali.
Alipelekwa Hospitali ya Palestina ambako baada ya kupimwa, alionekana kunywa pombe kali kupindukia, hivyo kuwekewa dripu.IMEANDALIWA NA: Chande Abdallah, Gladness Mallya, Shani Ramadhan, Mayasa Mariwata, Deogratius Mongela na Denis Mtima.