Eto’o
anaweza kuuhesabu 2014 kama mwaka mbaya kwake baada ya timu yake ya
taifa kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la dunia lakini pia hana
Club ya kuichezea baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, kama hiyo
haitoshi kwa sasa kilichombele yake ni kesi nzito Mahakamani.
Kesi hizo za udhalilishaji ni kutokana
na kusambaza picha za utupu, vitisho, ununuzi/uuzaji wa binadamu na
udanganyifu zimefunguliwa kwenye Mahakama moja jijini Yaounde, Cameroon
ambapo aliezifungua ni aliyekuwa mchumba wake wa zamani Hélène Nathalie
Koah.
Mapema
wiki iliyopita Koah alifungua kesi hizo dhidi ya Eto’o ambaye amekana
mashtaka hayo huku hili likiwa limetokea siku chache baada ya kusambaa
kwa picha zake za utupu kwenye mtandao Facebook ambazo mhudumu huyo wa
zamani wa ndege amesema zimesambazwa na Eto’o aliyekuwa mpenzi wake.
Eto’o amekanusha kuhusika na hilo na
katika kujibu mapigo mchezaji huyo anayeongoza kwa kutwaa tuzo nyingi za
uchezaji bora barani Afrika, amefungua kesi ya matumizi mabaya ya
fedha($410,755) alizompa Ms Koah kwa ajili ya kufungua taasisi ya
kusaidia jamii wakati walipokuwa wapenzi.