Stori: Gladness Mallya
JAPOKUWA
Mnenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Otilia Boniface alibadili dini na
kuwa Muislamu baada ya kupata mchumba ambaye ni muumini wa dini hiyo,
imebainika anatarajia kufunga ndoa ya bomani kutokana na ndugu zake
kutoridhika na uamuzi wake wa awali.
Akizungumzia hilo, Otilia alisema: “Ni kweli tutafunga ndoa ya bomani japokuwa tangu nilipoachana na mume wangu wa kwanza (Thabit) sikubadili dini tena, niko kwenye Uislamu na ndugu nao hawana hiyana kikubwa sasa wanamsubiri huyo mkwe wao.”