HUKU akiwa
kwenye vikao vya maandalizi ya harusi na Mzungu, staa wa filamu Bongo,
Lucy Francis Komba (pichani na mchumba wake), amejikuta katika wakati
mgumu baada ya habari kudai kwamba, mchumba wake huyo amemwambia ili
ndoa ifungwe lazima aoneshe cheti cha kipimo cha Ukimwi kwanza.
“Ukweli Lucy anahaha kutafuta cheti cha Ukimwi, mchumba anasubiri akione vinginevyo hawatafunga ndoa,” kilisema chanzo.
Ilidaiwa kuwa, mpaka sasa Lucy ameshafika kwenye hospitali tatu kubwa mbili, TMJ na Marie Stopes ili kufanya maarifa lakini imeshindikana.
Baada ya kupata habari hizo paparazi wetu alimtafuta Lucy ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Si kweli! Hao wanaosema hivyo ni wanafiki, sijui wanataka nini maana kila siku wanazusha mambo ya ajabu. Kwanza mimi huwa sitibiwagi kwenye hospitali hizo ulizozisema, natibiwa Regency.
Lucy Francis Komba.
“Kuhusu kupima Ukimwi, mimi na mchumba wangu tulishapima hukohuko kwao Ulaya (Denmark) ndiyo maana tukaanza taratibu za ndoa.“Namshangaa sana huyo aliyesema hayo hata kama ni mtu wangu wa karibu, mimi huwa simwelezi mtu mambo yangu binafsi kwa sababu duniani hakuna rafiki wa kweli, rafiki anakuchekea machoni lakini wote ni wabaya,” alisema Lucy.
Amani lilifika kwenye hospitali hizo lakini kukakosekana ushirikiano kwa madai kwamba, hakuna utaratibu wa kumtaja jina mgonjwa kama alikwenda kutibiwa.