Maiti ya kijana huyo ikiwa imenasa kaburini
ukio la ajabu
na la kushangaza limetokea huko nchini Nigeria baada ya kijana mmoja
kukutwa akiwa amekufa kaburini,kijana huyo alikumbwa na umauti wakati
akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili
ya matumizi ya mambo ya kishirikina.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Saturday Tribune wa Nigeria, tukio hilo limetokea
katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa
huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.Mmoja wa wakazi wa eneo
hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na marafiki zake wengine
waliokuwa wanafanya tukio hilo lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa
ndani ya kaburi walikimbia na kumuacha akihangaika kujinasua,lakini
jitihada zake ziligonga mwamba mpaka pale umauti ulipo mkuta.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi huku kichwa chake kikiwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hilo waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.

Mtandao
wa Saturday Tribune ulibaatika kuongea na kamishina wa Jeshi la Polisi
wa eneo la Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya
uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilipelekea
kijana huyo kupoteza maisha.
Msemaji
wa jeshi hilo aliongeza kuwa mpaka sasa jeshi lake bado halijathibisha
kwamba tukio hilo limetokana na masuala ya kishirikina.