STAA wa sinema za Kibongo, Nurdin
Mohammed ‘Chekibudi’ amejikuta ameingia kwenye bifu kali na mwigizaji
Helen Luanda ‘Zerishi’ baada ya mwanadada huyo kumtuhumu kuwa
amemdhulumu kazi yake ya filamu.Staa wa sinema za Kibongo, Nurdin Mohammed ‘Chekibudi’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Zerishi alisema aliamua kumshirikisha
Chekibudi kwenye kazi yake na kukubaliana naye ampelekee filamu yake
sokoni na kumlipa shilingi milioni nne baada ya filamu hiyo kuuzwa
lakini kaingia mitini.Alipotafutwa Chekibudi kuhusiana na madai hayo alikana kumdhulumu na kusema vitu vyote anavyo Zerishi isipokuwa demo anayo yeye.