Kinamama walio karibu na familia ya
marehemu Isabela Andrew aliyebakwa hadi kufa wakiangua kilio baada ya
kushuhudia mahali mwili wake ulipokutwa huko Area C mjini Dodoma jana.
Mwili wa msichana huyo ulikutwa ukiwa
umeharibika katika moja ya pagale, lililopo Area C, Dodoma Mjini na
paparazi alishuhudia ukitolewa hapo kwa machela huku polisi wakiwahoji
mashuhuda wa tukio hilo.
Dodoma. Mfanyakazi wa ndani, Isabella
Andrew (18), amefariki dunia na kifo chake kikidaiwa kusababishwa na
kubakwa na watu wasiojulikana.
Mwili wa msichana huyo ulikutwa ukiwa
umeharibika katika moja ya pagale, lililopo Area C, Dodoma Mjini na
mwandishi wetu alishuhudia ukitolewa hapo kwa machela huku polisi
wakiwahoji mashuhuda wa tukio hilo.
Mkazi wa Mtaa wa Kiwanja cha Ndege,
Jackson Coy aliyekuwa akiishi na binti huyo alisema msichana huyo
alipotea tangu Jumamosi iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David
Misime, alisema mwili huo uliokotwa jana saa mbili asubuhi na kwamba
polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.
Mwili huo ulibainika baada ya mama
mmoja, Rehema Msambile kufika katika pagale hilo alipokuwa akifuatilia
nyendo za mtoto wake ambaye juzi alipigwa kwa tabia ya utoro shuleni.
“Niliamua leo (jana) kumfuatilia, nikaanza katika mapagale.
Nilipofika hapa ndipo nikaona mwili wa marehemu ikabidi nimuite jirani hapo aje aone,” alisema.
Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege,
Henry Kandenga alisema mazingira yanaonyesha kuwa binti huyo alibakwa
kwa sababu walikuta nguo za ndani zikiwa pembeni.
“Hakuna yowe iliyosikika kwamba kuna mtu
anauawa ukizingatia kwamba nyumba ziko jirani na hata nyumba aliyokuwa
akiishi ni jirani na mahali alipokutwa,” alisema.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.