Na Rhoda Josiah
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka ameweka wazi kwamba kinachomfanya aishi vizuri na wenzake ni kutoendekeza makundi.
“Nampenda kila mtu na nipo tayari kuwa na urafiki na mtu yeyote atakayekuwa tayari kuwa karibu na mimi, makundi hayana maana kabisa zaidi ya majungu tu,” alisema Rose.